![]() |
Your community website |
![]() |
||||||
|
|
|
|||||||
|
|
||||||||
|
|
||||||||
|
|
||||||||
|
NEWS archive |
||||||||
|
27 December 2007 |
||||||||
Benazir Bhutto Auwawa
Benazir Bhutto ni mwanamke wa kwanza kuwa Waziri mkuu katika dola za kiislam. Alizaliwa mwaka 1953 na alimaliza masomo yake ya chuo kikuu Oxford, England mwaka 1977 na kumalizia masomo yake ya juu katika chuo kikuu cha Havard, USA. Bhutto alizaliwa katika kijiji cha Sindh. Wakati wa uwaziri wake kati ya mwaka 1988 na miaka ya mwanzo ya 90, alikuwa wakati mmoja na bibi Margaret Thatcher akiwa kama waziri wa UK. Uwaziri wake uliishia mwaka 1990 kwa maovu aliyoonekana nayo na mumewe ambayo yalikuwa ni kinyume na sheria. Akagombea tena uwaziri mwaka 1993 na kuchaguliwa mpaka mwaka 1996 mwisho wa uwaziri wake. Aliendelea kuishi Pakistan mpaka mwaka 1999 na kuamua kuhama nchi kwenda kuishi Dubai, kutokana na maneno yaliyomuandama kuhusu utajiri wake na mumewe. Benazir alijiamulia kuishi nje alivyoona mambo yanazidi kuwa mabaya Pakistan baada ya Pervez Musharaf kuchukua nchi kutoka kwa waziri mkuu wa zamani Nawaz Sharif. Benazir Bhutto alikutana na Nawaz Sharif kwa mara ya mwisho mjini London mwaka 2006. Mwaka 2007, Oktoba, Benazir Bhutto alichukua ndege kurudi zake Pakistan kugombea tena uwaziri mkuu katika serikali ambayo inayoendeshwa na General Pervez Musharraf. Katika kampeni zake za mwanzo, alikoswa na kuuliwa kwa bomu kusini mwa Karachi, ambalo bomu hilo liliua zaidi ya watu mia. Lakini Benazir Bhutto hakutishwa na vitisho hivyo na aliendelea na kampeni zake za kurudisha demokrasia nchini Pakistan. Baba yake Benazir Bhutto bwana Zulfikar Ali Bhutto alikuwa ni rais wa Pakistan wakati mmoja India ilivyokuwa ikiongozwa na Indira Gandhi.
|
||||||||
|
Custom Search
|
||||||||
|
|
|
|||||||
|
©
www.zenjydar.co.uk - Since 2007 |
|
||||||||