Kikwete akutana na mfalme
wa Qatar
01/12/2008

JK
akiongea na Emir wa f Qatar sheikh Hamad bin Khalifa al Thani hoteli ya
Four Seasons jijini Doha leo. JK yuko huko kuhudhuria mkutano wa fedha
na maendeleo.
Mtawala
wa Qatar, (The Emir His Highness Sheikh Hamad bin Khalifa Al Thani)
amesema kuwa wakati umefika kwa nchi za Afrika kubadilisha mawazo kwa
kutafuta mitaji ya uwekezaji katika nchi tajiri za Kiarabu, badala ya
kuendelea na jadi ya kusaka raslimali za maendeleo katika nchi za
Magharibi.
Mtawala
huyo wa Qatar pia ametaka hatua zaidi kuchukuliwa ili kuimarisha
uhusiano wa kihistoria kati ya nchi yake na Tanzania, akisisitiza kuwa
hata muziki, jadi na utamaduni wa nchi hizo mbili vinafanana.
Mtawala
huyo ameeleza hayo wakati alipomkaribisha na kufanya mazungumzo na Rais
Jakaya Mrisho Kikwete ambaye yuko Qatar kuhudhuria mkutano wa kimataifa
unaojadili jinsi ya kusaka fedha za kugharimia maendeleo na jinsi ya
kukabiliana na matatizo ya sasa katika mfumo wa fedha duniani.
|