Alexander Nyirenda -
Shujaa wa mwenge wa Uhuru
10/12/2008

Picha ya
kumbukumbu ya mwenge wa uhuru. Alexander Gwebe Nyirenda (pichani), ni
jina ambalo linakumbukwa na litaendelea kukumbukwa kutokana na mchango
wake hususani wakati wa sherehe za uhuru. Nyirenda ndiye aliyeipandisha
bendera ya uhuru kileleni katika Mlima Kilimanjaro na kuuwasha mwenge wa
uhuru ili umulike mipaka yote ya Tanganyika kwenye mkesha wa siku ya
uhuru wa Tanganyika Disemba 9, 1961.
|