Mount Kilimanjaro

Beit El Ajaib
     

HomeNewsServicesEventsAbout UsContact Us

 
ProfileToolsGamesCommunity

NEWS

 
 

Kupanda na kushuka kwa Air Tanzania

12/12/2008

Pichani ni moja ya ndege za Shirika la Ndege Tanzania ambalo sasa huduma zake zimesimamishwa. SHIRIKA la Ndege la Tanzania (ATCL), ambalo limekuwa na matatizo makubwa tangu ndoa yake ya Shirika la Ndege la Afrika Kusini (SAA) ivunjike, limenyang’anywa cheti cha kuruka angani na Mamlaka ya Anga (TCAA) baada ya kukosa viwango vya ubora kuruka angani.

Taarifa kutoka ndani ya ATCL zimeeleza kuwa shirika hilo limenyang’anywa cheti hicho tangu Disemba 8 mwaka huu na hivyo litashindwa kusafirisha abiria hadi hapo litakapokidhi masharti ya usalama wa anga ndipo itakaporejeshewa cheti hicho. Miongoni mwa viwango hivyo vya usalama ni ukaguzi wa mara kwa mara wa ndege zake, kuwa na wataalamu wa kutosha kama marubani na wahandisi, vitu ambavyo vimeonekana kukosekana kwenye shirika hilo la serikali.

Kufungiwa huko kumekuja huku kukiwa na uwezekano wa shirika hilo kufungiwa na Chama cha Kimataifa cha Usafiri wa Anga (IATA) kufanya safari zake baada ya kubaini zaidi ya makosa 500. Mwishoni mwa wiki iliripotiwa kuwa ATCL ilikaguliwa mwezi Oktoba na kubainika na makosa hayo ya usafiri wa anga, lakini ikashindwa kuyarekebisha na ndipo IATA ilipoanza mchakato wa kutaka kuizuia kufanya safari. “Ni kweli ATCL imenyang’anywa cheti cha viwango kwa kukosa ubora wa kuruka angani hivyo haitafanya safari za nje wala ndani ya nchi,” alisema mmoja wa watu wa ndani TCAA alipohojiwa.

Kwa mujibu wa taarifa hizo, ndege za ATCL zilizokuwa zikifanya safari zake ndani na nje ya nchi haitaweza kufanya tena safari hizo na vigogo wa ATCL jana walikuwa na vikao na TCAA kuzungumzia suala hilo. Alipoulizwa kuhusu suala hilo katibu mkuu wa Wizara ya Miundombinu, Omar Chambo alisema hana taarifa kuhusu kunyang’anywa cheti kwa ATCL na kudai kuwa mkurugenzi wa shirika hilo, David Mataka ndiye anayeweza kueleza suala hilo. “Sina taarifa kuhusu suala hilo... hayo ni mambo ya ATCL na anayeweza kukueleza ni Mataka, hivyo wasiliana naye... haiwezekani toka tarehe nane hadi leo mimi sijui,” alisema Chambo.

Kupozi au kuruka, ukweli utafichuka.

 

   
 

Custom Search

Go up

 

Quick Links

Watch Television
News Archive

© www.zenjydar.co.uk - Since 2007 | Web master | Site map | www.zenjydar.co.uk - Since 2007 ©