Sherehe za Eid-el-hajj
Festival 2008 (1429H)
14/12/2008

Baadhi ya Waislamu wanaozungumza Kiswahili
wa East London walijumuika pamoja katika kusheherekea sikukuu za
kuadhimisha kufaulu kwa nabii Ibrahim (A.S) baada ya kupewa mtihani na
Mwenyezi Mungu (S.W) wa kumchinja mwanawe nabii Ismail (A.S) na bila ya
kusita wote wawili walikubaliana na uamuzi huo mpaka Mwenyezi Mungu (S.W)
alipowashushia kondoo baada ya kuangalia nia waliyokuwa nayo ya kutimiza
maamrisho yake (S.W).

Pichani ni Munawwar Mussa, mtoto
anayechipukia katika jamii ya Kiswahili mwenye kuonyesha vipaji
alivyokuwa navyo, alifungua kwa kusoma Qur'an (suratul Imran aya ya 96
mpaka aya ya 109) na tafsiri yake na kufuatiwa na utenzi wake mbele ya
waliohudhuria katika hafla hiyo ya Eid-el-hajj Festival 2008
iliyoandaliwa na Zenjydar Community Association.

Katika kutimiza hafla hiyo, Zenjydar
ilialika jumuia zote za karibu za East London kujiunga kwa pamoja katika
kusheherekea sikukuu hiyo kubwa na kuweza kutunisha mifuko mbalimbali ya
maendeleo ya jumuia hizo. Pichani juu, Ustadh Hafidh Karama akiwakilisha East
African Education Foundation akiwa katika meza yake.
Baada ya mwaka wa jana jumuia ya East
African Education Foundation na jumuia ya Alnoor CET ya Barking
kushiriki kwa pamoja katika hafla ya Eid-el-hajj Festival iliyoandaliwa
na Zenjydar tarehe 23/12/2007, mwaka huu sherehe ya Eid-el-hajj
iliyoandaliwa na Zenjydar iligongana na sherehe ya Alnoor CET ya Barking
kutokana na jumuia zote mbili kukosa ukumbi siku ya Jumamosi ya tarehe
13/12/2008 (wikiendi ya mwanzo ya siku ya Eid-el-adhaa), lakini jumuia
zote zimejulishana hali hiyo na wote wamekuwa radhi kuendelea kufanya
siku moja kwa nia moja. Aidha, jumuia nyingine alikwa zilikutwa na
dharuri ya kutohudhuira katika hafla hiyo.

Nyota nyingine inayochipukia katika jamii
ya Kiswahili mtoto Omar Salum (kushoto) akiwa katika mchezo wa kuigiza
wa Kiislam, akiwa na muigizaji nyota chipukizi katika jamii ya Kiswahli
bwana Farid Nassor (kulia) ambao walionyesha ustadi wao katika mchezo
huo wa kuigiza ambao ulisisimua watu kwa majonzi na vicheko ambao
ulitungwa na kuendeshwa na bwana Saleh Jaber.

Omar Salum (kulia) na bwana Farid Nassor (kushoto)
wakionyesha umahiri wao kwenye steji.

Ana kwa ana bwana Farid Nassor (kulia)
ambaye alijulikana kwa jina la "Kikoi" akimueleza jambo Omar Salum
(kushoto) ambaye alijulikana kwa jina la "Kibandiko".

Bwana Kikoi (Farid Nassor) akionyesha
hisia zake kwa kumueleza jambo rafiki yake bwana Kibandiko (Omar Salum).

Bwana Kibandiko (Omar Salum) akinyosha
mikono juu na kusema aliyoyasema kwenye mchezo huo wa kuigiza wa Kiislam.

Bwana Kibandiko (Omar Salum) akionekana
akimuuguza rafiki yake bwana Kikoi (Farid Nassor) akiwa chini katika
mchezo wa kuigiza wa Kiislam.

Pichani ni waliohudhuria katika sherehe ya
Eid-el-hajj Festival 2008, kutoka kulia ni bwana Naher, akifuatiwa na
bwana Abdulkareem na mtoto wake Faiz, na kushoto Mheshimiwa bwana Said
Suleiman Omar.

Kutoka kulia ni bwana Salum Omar akiwa na
Aisha, na kushoto ni Mheshimiwa Ustadh Nassor Haroub (Mwenyekiti wa East
African Education Foundation).

Pichani kulia ni bwana Mussa akwa na
watoto wake Mundhir na Mahir ambao wakiwa katika mchanganyiko na waototo
wenzao waliofika katika hafla ya Eid-el-hajj Festival 2008.

Baadhi ya watoto wengine wakiwa katika
viti vyao wakipata chakula cha Urojo ambao ndio kilikuwa chakula maalum
cha sherehe hiyo "Special Urojo Evening".

Watoto waliofika katika sherehe hiyo
walikuwa katika hali ya urafiki na udugu.

Katika kuhitimisha sherehe ya Eid-el-hajj
Festival 2008, Zenjydar Community Association ilijitolea mchango wake wa
kukuza mfuko wa kuchangia jumuia ya Alnoor CET ya Barking na jumuia ya
East African Education Foundation katika miradi yao kwa kunadisha mnada
wa saa ya ukutani ambayo imesanifiwa vizuri kwa sanaa za Kiislam.
Baada ya vuta nikuvute ya mnada huo,
hatimaye bwana Omar Khaleef (pichani juu) alishinda saa hiyo na kuweza
kuichukua nyumbani kwake. Asilimia Hamsini ya pesa zote zilizopatikana
katika mnada huo zitakwenda katika mfuko wa Alnoor CET Barking na
Asilimia Hamsini itakwenda kwenye mfuko wa East African Education
Foundation.
Hongera bwana Omar Khaleef! Wabillahi
Tawfeeq.

Zenjydar Community Association inawatakia
wote sikukuu njema ya mwaka 2008 (1429H) na kheri za mwaka mpya 2009
(1430H).
|