Mount Kilimanjaro

Beit El Ajaib
     

HomeNewsServicesEventsAbout UsContact Us

 
ProfileToolsGamesCommunity

NEWS

 
 

Taifa Stars yaizamisha Nile Crocodiles ya Sudan 2-1

15/12/2008

Mkereketwa na mmoja wa viongozi wa kamati ya Saidia Stars Ishinde Dk. Ramadhani Dau naye alikuwepo toka Sudan na katika msafara ambapo alidanda juu ya gari toka Eapoti hadi mjini.

Ushindi wa Taifa Stars ambao iliupata Jumamosi kwenye Uwanja wa Al Hilal jijini Khartoum, Sudan, dhidi ya wenyeji Nile Crocodiles umefungua ukurasa mpya wa mpira wa miguu Tanzania kwani ni changamoto kwa michezo mingine kuwa pale ambapo wahusika wanapotimiza majukumu yao ipasavyo hakuna kisichowezekana.

Ni wazi kuwa mafanikio hayo si changamoto kwa wachezaji wa Taifa Stars watakaokwenda Ivory Coast katika fainali hizo zitakazoshirikisha timu nane, bali itakuwa vilevile kwa wachezaji chipukizi na wale wanaoinukia lakini hawafanikiwi kupata nafasi ya kuitwa kwenye timu hiyo.

Pia tunaupongeza uongozi mpya wa TFF uliochaguliwa katika uchaguzi uliofanyika Jumapili chini ya Rais Leodegar Tenga na makamu wake wawili Athuman Nyamlani na Ramadhan Nassib.

Uongozi huo una changamoto kubwa ya kulinda mafanikio yaliyopatikana na kutekeleza mengine ambayo hayakufanyika katika awamu iliyopita. Changamoto hiyo ni kubwa kwa vile wadau wana matumaini makubwa kutoka kwa safu hiyo mpya.

Lakini shukrani za pekee ni kwa wajumbe wa Mkutano Mkuu kwa kuchagua safu ambayo TASWA tuna imani kuwa ina nia, uwezo na sababu ya kukabidhiwa majukumu hayo hasa wakati huu ambapo hamasa katika mpira wa miguu hasa kwa timu ya Taifa imeanza kurudi.

Kocha Marcio Maximo wa Taifa Stars akionyesha alama ya ushindi wa mabao 2-1 kwa tabasamu kubwa.

 

   
 

Custom Search

Go up

 

Quick Links

Watch Television
News Archive

© www.zenjydar.co.uk - Since 2007 | Web master | Site map | www.zenjydar.co.uk - Since 2007 ©