Mount Kilimanjaro

Beit El Ajaib
     

HomeNewsServicesEventsAbout UsContact Us

 
ProfileToolsGamesCommunity

NEWS

 
 

Shujaa wa mwenge wa Uhuru kuzikwa leo

24/12/2008

Shujaa aliyepandisha Mwenge wa Uhuru kwenye kilele cha mlima Kilimanjaro siku ya mkesha wa uhuru wa Tanganyika, Disemba 9, 1961 amefariki dunia tarehe 20/12/2008 na kuzikwa leo kwenye makaburi ya Kinondoni, Dar es Salaam.

Nyirenda alizaliwa Tarehe 2 Februari 1936 Karonga, Malawi, wakati wazazi wake wakiwa katika likizo ndefu ya Krismasi kutoka Tanganyika. Alisoma shule ya msingi ya Mchikichini Dar es Salaam na baadae shule za Sekondari za wanaume za Malangali (mkoani Iringa) na Tabora, hadi 1957.

Baadhi ya waombolezaji wakisubiri mwili wa marehemu kuletwe kwa mazishi. toka shoto ni mzee Said El Maamry, Meja mstaafu Kashmir, Hamza Kasongo, George Kritsos na Kanali mstaafu Julius Mbilinyi. Alietupa mgongo hakuweza kutambulika mara moja.

 

   
 

Custom Search

Go up

 

Quick Links

Watch Television
News Archive

© www.zenjydar.co.uk - Since 2007 | Web master | Site map | www.zenjydar.co.uk - Since 2007 ©