Mali za ATCL (Air
Tanzania) zakamatwa
31/12/2008

Pichani ni Moja ya gari la Kampuni ya
Ndege Tanzania (ATCL) linaloshikiliwa na Benki ya Stanbic Tanzania,
likiwa limeegeshwa katika Makao Makuu ya benki hiyo, Dar es Salaam
Benki ya Stanbic Tanzania Limited, Makao
Makuu ya Kinondoni, Dar es Salaam, inayashikilia magari sita ya Kampuni
ya Ndege Tanzania (ATCL), baada ya kushindwa kulipa deni la Sh bilioni
mbili iliyochukua kama mkopo. Fedha hizo zinazodaiwa kushindwa kulipwa
kwa miezi miwili sasa zilikopwa na wafanyakazi wa kampuni kwa mikopo na
kutokana na kushindwa kuwalipa mishahara watumishi wake, makato ya kila
mwezi yameshindikana kukatwa.
Taarifa zilizopatikana kutoka ATCL na
katika benki hiyo jana zilithibitisha kushikiliwa kwa magari matano aina
ya Toyota Land Cruiser VX, na gari la sita limekamatwa likiwa mjini
Moshi, Kilimanjaro na lilipelekwa katika benki hiyo jana na kufanya
idadi ya magari hayo kuwa sita.
Waandishi wa habari walitaka habari zaidi
kwa undani, lakini uongozi wa benki uliokuwapo haukuwa tayari kuzungumza
kwa madai kuwa msemaji wa benki hiyo yupo likizo.
Aidha, inasemekana ndege za ATCL
zimefunguliwa mbawa zake kuanza kazi ya kurusha abiria, lakini
wafanyakazi wamekosa mshiko wa mwezi mzima wa Disemba.
|