Serikali yapitisha £18
MILIONI kunawirisha kata ya Canning Town
01/11/2008

Serikali ya UK imepitisha £18 milioni
kuipatia mamlaka ya bara la Newham kwa madhumuni ya ujenzi wa
kunawirisha sura ya kata ya Canning Town, bara la Newham, East London,
bara ambalo Olimpik ya 2012 London itakapofanyika.
Moja ya sehemu maalumu ambayo ujenzi huo
utaanza kufanyika ni barabara ya A13 ambayo ni barabara kubwa
inayounganisha wakazi wa Newham kutoka nje na ndani ya bara la Newham.
Diwani Conor McAuley amesema, hii ni
habari nzuri kwasababu barabara kubwa ya A13 na mduara wa Canning Town
ndio kitovu cha magari yanayotoka katikati ya London, Custom House na
pande zingine ambapo kwa sasa imeshaanza kuonyesha ugumu wa usafiri
kupitia hapo kutokana na wingi wa magari yanayotumia njia hiyo. Vilevile
itasaidia kuunganisha watu wa Newham ambao wamegawishwa pande mbili (kusini
na kaskazini) kwasababu ya barabara hiyo kubwa ya A13.
The London Thames Gateway Development
Corporation inafanya kazi pamoja na mamlaka ya bara la Newham katika
ujenzi huo ambao wamesanii kuwa na sehemu nzuri za matembezi kwa watu,
maduka, nyumba za kisasa na maeneo ya biashara.
Usanii wa kuitoa raundiabauti (roundabout)
ya A13 ambayo ipo katika kiungo cha A13 na Barking Road imeshaanza.
Raundiabauti hiyo itatolewa na kutakuwa na madaraja ya kuunganisha pande
zote mbili kwa waendao kwa miguu na wanaosafiri na vyombo vya usafiri.
Ujenzi huo unatarajiwa kuisha mwezi wa
tisa (Septemba) 2011.
|