NEWHAM yawakaribisha
wawakilishi wa UAE
03/11/2008

Bara la Newham, East London
limewakaribisha wawakilishi 11 (kumi na moja) wa kutoka serikali ya dola
za Kiarabu (UAE).
Mualiko huo rasmi, umeandaliwa na SLG
(Shared Leadership Group) shirika la kuangalia miundo mbinu ya
teknolojia ambayo inaendelezwa kwenye mamlaka za serikali. Wadhamini wa
maandalizi hayo na mkutano huo walikuwa ni shirika kubwa duniani
(MICROSOFT) ambalo ni baba wa teknolojia za kisasa.
Wawakilishi hao wamefika katika kudurusu
na kuangalia vipi serikali za UK zinaendeleza teknolojia yake kwenye
sekta za huduma za raia vilevile UAE ikiwa ni moja ya nchi zinaazoongoza
katika mambo ya ujenzi duniani, wawakilishi hao watafaidika kuangalia
vipi Newham imeandaa katika maendeleo ya kiteknolojia ya ujenzi kwa
maandalizi ya Olimpik 2012.
Wawakilishi hao wanatarajiwa kudurusu
sehemu mbalimbali za teknolojia na kuchukua teknolojia hiyo nyumbani
kwao katika maendeleo mbalimbali ya nchini UAE.
|