Teknolojia mpya ya
kuzalisha umeme
14/11/2008

Teknolojia mpya ya kuzalisha umeme jijini
London kwa njia ya matuta ya barabarani (Road Humps) ipo katika
majaribio ambayo ni ya kwanza aina yake duniani.
Mamlaka ya Ealing, London imepewa madaraka
ya kufanya majaribio hayo kwa kupitisha gari za Polisi juu ya matuta
hayo (pichani).
Kila mara gari inapopita juu ya matuta
hayo yanakuwa yanasababisha 'pressure' ambayo inazalisha umeme.
Umeme unaozalishwa kwa nguvu ya uzito wa
gari yapitayo kwenye matuta, utakuwa unatumika kuendeshea taa za
barabarani za usalama (Street Lights, Traffic Lights na Road Signs).
Majaribio hayo yakiwa na matokeo mazuri,
teknolojia hiyo itaendelezwa kutumiwa mji mzima wa London.
Muwakilishi wa Ealing alisema, chini ya
matuta hayo kuna vitu kama sahani ambazo sahani hizo zinagusana gari
inapopita juu na kusababisha nguvu ya umeme.
Kila tuta moja kutengeneza linagharimu
£50,000.00 (elfu hamsini), pesa hizo zinalipwa na mamlaka ya usafiri wa
London (Transport for London).
Vilevile alisema muwakilishi huyo, matuta
hayo yanaweza (kupanda na kushuka) kupandishwa kuwa kama kigezo cha
kupunguzia magari kasi au yanaweza kushushwa na hata madereva wasihisi
kama wanapita juu ya matuta.
|