Mama Maria Nyerere akutana
na Waziri wa Msumbiji
29/11/2008

Mama Maria Nyerere akimpa
maelekezo Waziri Mkuu wa Msumbiji Luisa Diogo (aliyevaa nguo ya rangi ya
udongo) kuhusiana na aina ya mboga iliyopo katika bustani yake.

Waziri Mkuu wa Msumbiji
Luisa Diogo pamoja na wageni wengine wakitembelea bustani ya mboga ya
Mama Maria Nyerere wakati walipomtembelea nyumbani kwake Msasani Jijini
Dar es Salaam.

Waziri Mkuu wa Msumbiji
Luisa Diogo akibadilishana mawazo na Mama Maria Nyerere.

Waziri Mkuu wa Msumbiji
Luisa Diogo akimvisha zawadi ya nguo aina ya kikoi Mama Maria Nyerere
wakati alipomtembelea nyumbani kwake Msasani.

Waziri Mkuu wa Msumbiji Mh.
Luisa Diogo na Mama Maria Nyerere wakati alipomtembelea nyumbani kwake
Msasani Jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kumjulia hali.
|