Mount Kilimanjaro

 

 

 

Your community website

Beit El Ajaib
     

HomeNewsServicesEventsAbout UsContact Us

ProfileToolsGamesCommunity

NEWS

 
 

UHURU HEIGHTS kukwangua anga za Dar es Salaam

04/08/2008

Jengo la Uhuru Heights limesanifiwa kuwa jengo refu nchini mahsusi kwa ajili ya biashara na makazi. Kivutio hicho cha jengo kimebeba nembo ya mwenge wa uhuru ambao uliwekwa kwenye kilele cha Mlima Kilimanjaro. Jengo hilo la Uhuru Heights ni mradi muhimu kwa ajili ya kuifanya mitaji ya biashara na lipo sehemu nzuri kwenye Barabara ya Bibi Titi Mohammed katikati ya jji eneo la Upanga na OysterBay.

Jengo hili litajengwa mbele ya bahari na litaweza kutoa fursa kwa watu kutazama na kupata upepo wa bahari ya Hindi na litakuwa na vifaa vilivyotengenezwa kwa ubora unaokubaliaka duniani. Eneo litakapojengwa ni zuri na litavutia kibiashara. Ghorofa tano ndani ya jengo zitakuwa ni kwa ajili ya ofisi zenye ukubwa tofauti.

Usanifu wa jengo na umaliziaji wa hali ya juu kutawezesha na kukidhi uendeshaji wa shughuli kama vile kuunganishwa na Intaneti iliyo na kasi kubwa, maegesho na ulinzi kwa saa 2.

Jengo hili litakuwa na ghorofa 25 litakuwa ni eneo la kuvutia,likiwa na burudani na mambo mengine ya kuvutia katika maisha ya jamii. Duka la nguo za mitindo ya aina mbalimbali litakuwa kwenye mwanzo wa jengo chini na kwenye ghorofa ya kwanza na litaonyesha mitindo mbalimbali inayopongoza kwa ubora duniani. Ghorofa ya pili itakuwa na mgahawa ambao utakuwa ni wa kipekee utakaokuwa na mchanganyiko wa vyakula kutoka tamaduni mbalimbali na utahudumia wateja kutoka mataifa mbalimbali sanjari na ukumbi mkubwa wa chakula.

Ukumbi wa burudani utakuwa na eneo la michezo mbalimbali ya watoto na ukumbi wa michezo.Kwenye maeneo ya makazi ya jengo hilo kutakuwa na bwawa la kuogelea na sehemu ya kufanyia mazoezi ya viungo (gym) kwa ajili ya wanawake na wanaume,eneo lamichezo kwa ajili ya watoto na ukumbi wa sherehe ambao unaweza kuchukua watu 100 hadi 120.

 

   
 

Custom Search

Go up

 

Quick Links

Watch Television
Events Calendar
News Archive 2008
News Archive 2007

External Links

Alnoor CET
TZ Embassy UK
TZ's Community UK

© www.zenjydar.co.uk - Since 2007 | Web master | Site map | www.zenjydar.co.uk - Since 2007 ©