Mount Kilimanjaro

 

 

 

Your community website

Beit El Ajaib
     

HomeNewsServicesEventsAbout UsContact Us

ProfileToolsGamesCommunity

NEWS

 
 

Angela Luballa arudisha taji la Redds kwa imani ya dini

10/08/2008

Pichani (kushoto) ni Meneja wa kinywaji cha Redds George Kavishe alipokuwa akimtambulisha balozi mpya wa kinywaji cha Redds, Angela Luballa (kulia), kati ni balozi wa kinywaji cha Redds aliyemaliza muda wake Victoria Martin.

Mshindi wa taji la Balozi wa Redd’ katika mashindano ya Miss Tanzania mwaka huu, Angela Luballa amevua taji hilo na kurudisha kwa waandaaji.

Akizungumza jijini Dar jana, Angela alisema amechukua uamuzi huo kutokana na imani yake ya dini ya Kikristo, ambapo yeye anaabudu kanisa liitwalo World Alive International Outreach lililopo Sinza, jijni Dar.

Alisema amefikia uamuzi huo bila kushawishiwa na mtu na anaona halitakuwa jambo la busara kuendelea kuwa Balozi wa kinywaji cha Redds, wakati imani ya dini yake haimruhusu.

“Nachukua fursa hii kuiambia jamii kuwa kutokana na imani yangu katika Yesu Kristo, sitaweza kuwakilisha Redds kama Redds Fashion Ambassador 2008.

“Kwa kuwa mimi si mbinafsi, narudisha taji hili na zawadi zake zote kwa Redds, napenda kutoa shukrani zangu za dhati kwa Vodacom, Lino na Redds kwa uelewa juu ya uamuzi wangu huu”, alisema. Vodacom ndio wadhamini wakuu wa Miss Tanzania. Angela ambaye pia ni Miss Temeke 2008, alisema zawadi anayorudisha ni fedha sh. Milioni 2.5. Alipoulizwa kama hakujua wakati anashiriki mashindano hayo tangu mwanzo kama kuna jambo kama hilo, alisisitiza kuwa suala la kuwa Balozi wa kinywaji hicho haliendani na imani yake.

Angela (katikati) akiwa na wazazi wake.

 

   
 

Custom Search

Go up

 

Quick Links

Watch Television
Events Calendar
News Archive 2008
News Archive 2007

External Links

Alnoor CET
TZ Embassy UK
TZ's Community UK

© www.zenjydar.co.uk - Since 2007 | Web master | Site map | www.zenjydar.co.uk - Since 2007 ©