Mount Kilimanjaro

 

 

 

Your community website

Beit El Ajaib
     

HomeNewsServicesEventsAbout UsContact Us

ProfileToolsGamesCommunity

NEWS

 
 

Kikwete azindua ujenzi wa Machinga Complex

14/08/2008

Rais Jakaya Kikwete akizindua rasmi Ujenzi wa jengo la ghorofa sita eneo la Uwanja wa Karume, Ilala, jijini Dar es Salaam ambalo limejngwa maalum kabisa kwa wafanyabiashara ndogondogo wa jijini Maarufu kama Wamachinga.

Mwonekano wa Jengo la Ghorofa sita linalojengwa Uwanja wa Karume, Ilala, jijini Dar es Salaam Maalum kabisa kwa wafanyabiashara ndogondogo Maarufu kama Machinga.

HABARI KAMILI:

RAIS Jakaya Kikwete ameagiza huduma za kijamii zipelekwe nje ya Jiji,ili kuepusha msongamano.Rais alisema hayo leo asubuhi wakati akiweka jiwe la msingi katika Machinga Complex Ilala dar es Salaam.Jengo hilo linaendelea kujengwa.

Machinga Complex inayojengwa na uongozi wa Jiji la Dar es Salaam pamoja na Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF) ni wazo la Kikwete alilolitoa mwaka 2005 mjini Dodoma.

Rais alisema kutokana na msongamano uliopo jijini,haina maana tena kufikiria kujenga jengo kubwa kama hilo tena mjini.Jengo hilo lililopo Mtaa wa Lindi,Ilala Dar es Salaam.“Mkilazimika kubomoa nyumba,bomoeni tu,mradi utaratibu unafuatwa wa kisheria na kijamii,lakini lazima tukubali kwamba mji unakua na katika maendeleo yoyote ni lazima upande mmoja upate msukosuko,kusemwa,lakini matunda ndiyo kama haya,”alisema.

Aliwataka watendaji wasiogope maneno yanayoandikwa ama yatakayoandikwa magazetini kutokana na hatua mbalimbali watakazochukua kwa ajili ya upanuzi wa mji, lakini akawaonya tabia ya kuwahamisha watu kwenda nje ya miji bila kuwapatia huduma siyo sawa.“Mnawapeleka watu Bunju,Tuangoma,lakini hamfikirii hao watu watatibiwa wapi,maji yako vipi,umeme hampeleki halafu mnawalazimisha waondoke waende huko,hii si sawa,pelekeni huduma za kijamii nje,lakini ziambatane na miundombinu bora,”alisisitiza Rais.

Aliuagiza uongozi wa Jiji chini ya Meya wake Adam Kimbisa,kuhakikisha kuwa majengo mengine madogo kuliko hilo lenye uwezo wa kuchukua wafanyabiashara 10,000 yanajengwa katika Manispaa ya Temeke na Kinondoni,pia kutaka uwazi ufanyike wakati wa ugawaji wa maeneo ya biashara. Picha zote na Mdau Athuman Hamisi.

 

   
 

Custom Search

Go up

 

Quick Links

Watch Television
Events Calendar
News Archive 2008
News Archive 2007

External Links

Alnoor CET
TZ Embassy UK
TZ's Community UK

© www.zenjydar.co.uk - Since 2007 | Web master | Site map | www.zenjydar.co.uk - Since 2007 ©