![]() |
Your community website |
![]() |
||||||
|
|
|
|||||||
|
|
||||||||
|
|
||||||||
|
|
||||||||
|
NEWS |
||||||||
|
|
||||||||
Gazeti la Newham lamulika mwanga Timu ya Zenjydar15/08/2008
Baadhi ya vijana wa timu ya Zenjydar Community Association (pichani) wakidodesha medali zao walizozawadiwa katika mashindano ya bara la Newham, bara litakalofanyiwa michezo ya Olimpik 2012 mjini London. Vijana wa timu ya Zenjydar walishiriki katika mashindano ya kata za Newham na kubahatika kufika hadi nusu fainali. Timu ya vijana kama wangeshinda nusu fainali, wangebahatika kuchuana na mpinzani wao na kuonyesha ujuzi wao katika uwanja maarufu wa West Ham United uliopo Green Street, Newham, London. Mwenyekiti wa Zenjydar, bwana Saleh Jaber ambaye ni mvumbuzi wa GAP PROJECT amewapongeza vijana hao ambao wamewakilisha na kuwalete sifa jamii yao ya Waswahili katika kushiriki kwenye mashindano hayo. Vilevile, GAP PROJECT inasaidia vijana kuwa na afya kimwili na kiakili wanapokuja kufanya mazoezi na wenzao kwenye mandhari nzuri na kuepuka na fikra chafu au za uovu wanapokuwa mitaani au penginepo wasipoonekana kwa wakati ule baada ya masomo yao. Gazeti maarufu la bara Newham ambalo linaitwa Newham Mag limemulika mwanga wake kwenye timu ya Zenjydar na GAP project kuwekwa kwenye uso wa Newham kwa mchango wa Waswahili wanaochangia katika kuleta moja ya maendeleo katika bara hilo. bonyeza picha hii uone ukurasa uliojitokeza kwenye gazeti la Newham na maelezo yake.
Vijana hao hufanya mazoezi yao West Ham Park kila Jumamosi 9:30am mpaka 12pm na Jumapili 2:30pm mpaka 5:30pm (siku za kiangazi au summer). Tarehe 31/08/2008 itakuwa ni siku ya mwisho kwa kuupisha mwezi mtukufu wa Ramadhan na mazoezi yataanza tena tarehe 11/10/2008, saa kama kawaida.
|
||||||||
|
Custom Search
|
||||||||
|
|
|
|||||||
|
©
www.zenjydar.co.uk - Since 2007 |
|
||||||||