![]() |
Your community website |
![]() |
||||||
|
|
|
|||||||
|
|
||||||||
|
|
||||||||
|
|
||||||||
|
NEWS |
||||||||
|
|
||||||||
Je, huyu ni wewe?18/08/2008
Pichani ni Kondakta wa Basi linalofanya safari zake jijini Dar es Salaam akiongoza magari baada ya foleni kubwa ya kwenye makutano ya barabara ya Lumumba na Uhuru. Kujitolea kwa kondakta huyo kati ya Makondakta wote waliokuwapo hapo, ni moja ya kazi ya kila raia wa nchi kujitolea wakati jambo au mambo yoyote yanayojitokeza aidha kwa bahati mbaya, bila ya makusudio au kwa makusudio. Kujitolea kusawazisha ya wenzako au kusawazisha kwenye kila jambo linaloelekea pabaya ni haki ya kila raia kumshauri raia mwenzako ili ndugu au jamii au kijiji au nchi isielekee pabaya. Kwa nchi kama Uingereza wanaita "Duty of Care". Je, huyu ni wewe? Kwa yeyote anayemjua kijana huyo (pichani) atume namba yake ya simu, email: zenjydar@gmail.com na tuna zawadi ndogo tu ya kumpa ndugu yetu huyo mwenye mfano mzuri, ahsante. Zenjydar Community Association inawatakia Watanzania wote duniani, RAMADHAN KAREEM. Mhariri, Zenjydar Community Association
|
||||||||
|
Custom Search
|
||||||||
|
|
|
|||||||
|
©
www.zenjydar.co.uk - Since 2007 |
|
||||||||