Mount Kilimanjaro

 

 

 

Your community website

Beit El Ajaib
     

HomeNewsServicesEventsAbout UsContact Us

ProfileToolsGamesCommunity

NEWS

 
 

Uwekezaji wasisitizwa Ughaibuni

03/07/2008

Balozi Mh. Mwanaidi Maajar akimkaribisha Bw. Issa Omar atoe mada yake juu ya ujasirimali.

Bw. Omar akihutubia umati wa wajasiriamali waliofika kwenye mkutano huo.

Mwenyekiti wa jumjuiya ya Watanzania waishio Uingereza Mh. Abubakar Faraj akitoa hotuba.

Baadhi ya Watanzania waliofika katika mkutano huo.

Wajasirimali waliofika katika mkutano katika jengo la Ubalozi wa Tanzania, London, Uingereza (Tanzania House), wakisikiliza jambo katika hotuba iliyotolewa ya kuwahimiza Watanzania kuwekeza nyumbani, Tanzania.

Bw. Issa aliainisha fursa nyingi za biashara zilizopo Tanzania baada ya Serikali kufungua milango zaidi ya uwekezaji na kupatikana kwa wawekezaji wakubwa wa Kimataifa.

Akifafanua zaidi mtaalam huyo alisema hivi sasa takwimu zinaonyesha kuwa Tanzania inahitaji zaidi biashara za uwezo wa kati (medium enterprises) ili kuziba pengo kubwa kati ya wafanyabiashara wakubwa na wadogo. Alisema ili kuendelea zaidi kiuchumi, makampuni makubwa yanahitaji sana makampuni ya kati kwa ajili ya kutengeneza mali ghafi, kuzalisha nguvu kazi na kutoa ushauri wa kitaaluma.

Katika Mkutano huo ulihudhuriwa na Watanzania zaidi ya 30, Bw. Issa aliwashauri wajasiriamali hao kubuni miradi mbalimbali itakayowawezesha kupata mikopo kwenye benki za Tanzania ili kuweza kuanzisha biashara huko nyumbani. Aliwapa changamoto kuangalia fursa za biashara za huduma na ushauri wa kitaaluma.

Alisema benki nyingi hivi sasa nchini Tanzania zinawatafuta wenye miradi ya uhakika ili kuwakopesha mitaji ya kufanya biashara nchini humo. Alisema kwa elimu, upeo na uzoefu waliokuwa nao, wajasiriamali hao wanaweza kuanzisha miradi mizuri itakayowezesha kuinua uchumi wa Tanzania.

Kwa mafanikio zaidi, Bw. Issa amewashauri wajasiriamali hao kujiunga katika vikundi ili kuweza kujumuisha utaalam na mitaji ya msingi ya kuanzisha miradi hiyo. Alisema biashara nzuri inahitaji utafiti wa soko, udhibiti na shauku ya maendeleo zaidi.

Katika maswali yao kwa mtoa mada, wajasiriamali hao walipenda kufahamu mipango zaidi ya Serikali kuondoa urasimu. Bw. Issa aliwaambia kwamba wakati Serikali inaendelea na hatua mbalimbali kurekebisha mazingira ya uwekezaji na biashara nchini Tanzania, ni vyema Watanzania hao pia kutimiza wajibu wao badala ya kukaa tu kusubiri Serikali kufanya kila kitu. Alifafanua kwamba Watanzania walioko nje ya nchi wana uwezo mkubwa sana wa kubadilisha mazingira ya uwekezaji kama watarudi nyumbani na kuingiza utamaduni mpya wa kikazi.

Awali akimkaribisha mtoa mada, Balozi Mwanaidi Sinare Maajar alisema kwamba Ubalozi hivi sasa unafanya jitihada za kuwaunganisha wajasiriamali wa Kitanzania wa ngazi zote walioko Uingereza ili kuwashirikisha kikamilifu na Baraza la Biashara la Tanzania (Tanzania Business Council).

Bw. Issa yupo London kwa ajili ya Mkutano wa Uwekezaji wa Africa (Africa Business Forum 2008) ulioandaliwa na Commonwealth Business Forum.

 

   
 

Custom Search

Go up

 

Quick Links

Watch Television
Events Calendar
News Archive 2008
News Archive 2007

External Links

Alnoor CET
TZ Embassy UK
TZ's Community UK

© www.zenjydar.co.uk - Since 2007 | Web master | Site map | www.zenjydar.co.uk - Since 2007 ©