Mount Kilimanjaro

 

 

 

Your community website

Beit El Ajaib
     

HomeNewsServicesEventsAbout UsContact Us

ProfileToolsGamesCommunity

NEWS

 
 

Wauza DVD feki kukiona!!!

06/07/2008

Vijana wawili ambao wanauza DVD zisizo halali, ambao soko lao kubwa lilikuwa East Ham, katika bara la Newham, London, wamefikishwa mahakamani Stratford Magistrate Court, kwa tuhuma ya kuuza DVD zisizo halali kwa kukiuka sheria ya kifungu 92 cha hakimiliki (Trade Mark Act 1994).

Vijana hao, Da Hua Weng (34) na He Hua Jing (33) wakazi wa Tanners Hill, Lewisham, South East London, wamekamatwa baada ya ushirikiano mkubwa kati ya Newham Council na Metropolitan Police.

Weng, amehukumiwa kifungo cha siku 90 na kupigwa marufuku kufanya biashara ya aina yoyote kwa muda wa miaka 2, na marufuku kutoonekana katika mitaa ya High Street North, East Ham, kati ya Barking Road na East Ham Station.

Jing, ameachiwa kwa masharti maalum kwa muda wa miezi 24 (miaka 2) asionekane kwenye mitaa ya Newham akizurura ovyo au akiuza DVD zisizo halali.

Weng na Jing wote wamehukumiwa kwa kuleta usumbufu kwa watu kwa kuwang'ang'ania kununua DVD zisizo halali ambazo nyingineza zikiwemo DVD chafu.

Diwani June Leitch wa Newham amesema, watu huona kununua DVD hizi ni rai nzuri kwasababu ni rahisi, lakini filamu zake hazina hisia nzuri ya filamu halisi kwasababu filamu hizi huwa zinarekodiwa nyuma ya mabanda ya sinema na picha yake inakuwa si ya kusisimua. Alisema, ukiwa unatazama filamu hizo mara utasikia watu wakipiga chafya, wengine wakicheka na wengine hupita mbele ya kamera inayorekodi nyuma ya sinema.

Aliongeza kwa kusema, DVD hizi ni moja ya kosa la JINAI (Organised Crime), kwasababu wauzaji wanachokitaka ni pesa na hufikia hata kuuzia watoto wadogo DVD ambazo si halali na chafu kuzitizama.

Kasisitiza kwa kusema ni bora watu waende Sinema au kununua filamu kutoka maduka yanayoaminika kihalali.

 

   
 

Custom Search

Go up

 

Quick Links

Watch Television
Events Calendar
News Archive 2008
News Archive 2007

External Links

Alnoor CET
TZ Embassy UK
TZ's Community UK

© www.zenjydar.co.uk - Since 2007 | Web master | Site map | www.zenjydar.co.uk - Since 2007 ©