Mount Kilimanjaro

 

 

 

Your community website

Beit El Ajaib
     

HomeNewsServicesEventsAbout UsContact Us

ProfileToolsGamesCommunity

NEWS

 
 

Universal Studios yaungua moto

01/06/2008

Jumba maarufu la filamu duniani, Universal Studios, ambalo limezalisha filamu kubwa kubwa nzuri, limeteketea na moto usiku wa kuamkia leo.

Moto huo umeteketeza sehemu tofauti ndani ya jumba hilo ikiwemo sehemu inayowakilisha filamu maarufu ya 'Back to the Future" na vilevile sanamu kubwa la King Kong.

Moshi wa moto huo ulitanda na kuonekana mji mzima wa Hollywood, Los Angeles. Wanazimamoto 400 walikuwa katika kupigana na moto huo ambao mwisho wameweza kufanikiwa.

Inasemekana, karibu video 50,000 zilizohifadhiwa humo zimeungua. Na bahati mikanda ya filamu nyingine ilipona chupu chupu kwa kuwa ilikuwa ndani ya kabati la chuma.

Lakini, Rais wa Universal Studios, Ron Meyer amesema, mikanda yote ambayo imeungua, ina kopi zake ambazo zimehifadhiwa sehemu nyingine kuepukana na hali kama hiyo kutokea.

Katika moto huo, hakuna majeruhi wala mtu aliyepatwa na moto huo.

Ukubwa wa uwanja wa Universal Studios unafika eka 230.

 

   
 

Custom Search

Go up

 

Quick Links

Watch Television
Events Calendar
News Archive 2008
News Archive 2007

External Links

Alnoor CET
TZ Embassy UK
TZ's Community UK

© www.zenjydar.co.uk - Since 2007 | Web master | Site map | www.zenjydar.co.uk - Since 2007 ©