Mount Kilimanjaro

 

 

 

Your community website

Beit El Ajaib
     

HomeNewsServicesEventsAbout UsContact Us

ProfileToolsGamesCommunity

NEWS

 
 

Mkutano wa 8 wa Leon Sullivan umeanza rasmi

03/06/2008

Mkutano wa 8 wa Leon Sullivan umeanza rasmi katika ukumbi wa Arusha International Conference Centre (AICC) mjini Arusha, Tanzania, ambao utachukua siku tatu kuanzia Jumanne mpaka Alhamisi.

Rais Kikwete (pichani juu) alifungua mkutano huo kwa hotuba ya kuvutia na ya uchangamfu ambayo ilipamba rasilimali ambazo tunazo Tanzania na vilevile kuwashukuru wote ambao wamehudhuria katika mkutano huo ambao wametoka nchi za mbali.

Mkutano huo unaonyeshwa laivu kutoka Arusha na kanati ya TBC ya Tanzania kwa kupitia teknoloji ya vyombo vya habari.

Wasanii na watu maarufu wa kutoka fani mbalimbali wa Marekani, walihudhuria katika mkutano huo wakiwamo Chris Tucker, Jessey Jackson, na kadhalika...

Kaka Michuzi (kushoto) akiwa na msanii maarufu duniani Chris Tucker, ambaye hujulikana kwa umaarufu wake kwenye fani ya filamu mbalimbali za Hollywood.

Mchungaji Jesse Jackson akiwa katika banda la Daily News na Habari Leo kwenye maonyesho ya Sullivan na kufurahishwa na hazina kubwa ya picha za kumbukumbu zikiwamo zake yeye na za mastaa wengine wa Marekani.

Hotuba kamili ya ufunguzi ya Rais wa Tanzania, Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete bonyeza hapa

 

   
 

Custom Search

Go up

 

Quick Links

Watch Television
Events Calendar
News Archive 2008
News Archive 2007

External Links

Alnoor CET
TZ Embassy UK
TZ's Community UK

© www.zenjydar.co.uk - Since 2007 | Web master | Site map | www.zenjydar.co.uk - Since 2007 ©