![]() |
Your community website |
![]() |
||||||
|
|
|
|||||||
|
|
||||||||
|
|
||||||||
|
|
||||||||
|
NEWS |
||||||||
|
|
||||||||
Timu ya Manor Park yapambana na timu ya Hounslow07/06/2008
Timu ya Manor Park (rangi ya chungwa) ilipambana na timu ya Hounslow (rangi ya njano) katika mechi ya kirafiki ambayo ilifanyika katika uwanja wa Mayesbrook Park, Barking.
Ilikuwa vuta ni kuvute na timu zote zilionyesha ari ya kushinda mechi hiyo.
Timu ya Manor Park ikiwa katika kipindi cha mapumziko wakibadilishana mawazo na mbinu za kuwashinda wageni wao timu ya Hounslow. Kapteni wa mechi hiyo kwa upande wa Manor Park, SWITI (jezi ya kijani) akisaidia mbinu za ushindi.
Timu ya Hounslow ikiwa katika kipindi cha mapumziko wakibadilishana mawazo na mbinu za kuwashinda wenyeji wao timu ya Manor Park. Mpaka kufikia wakati wa mapumziko Hounslow ilikuwa ikiongoza bao 1-0. Kocha wa mechi hiyo kwa upande wa Hounslow, YASIR (jaketi la njano na nyeusi) akisaidia kutoa mbinu za ushindi.
Baada ya vuta nikuvute ya dakika tisini, timu ya Hounslow imewafunga wenyeji wao timu ya Manor Park kwa mabao 3-0.
|
||||||||
|
Custom Search
|
||||||||
|
|
|
|||||||
|
©
www.zenjydar.co.uk - Since 2007 |
|
||||||||