![]() |
Your community website |
![]() |
||||||
|
|
|
|||||||
|
|
||||||||
|
|
||||||||
|
|
||||||||
|
NEWS |
||||||||
|
|
||||||||
Mgomo wa Daladala - Dar es Salaam08/06/2008
Hivi karibuni magari ya abiria (Daladala) jijini Dar yalitangaza mgomo wa kusimamisha huduma zao za kusafirisha abiria kwa kile walichodai kuwa bei ya mafuta imepanda hivyo na nauli ipandishwe. Kufuatia kauli hiyo pia mkuu wa mkoa wa jijini Dar, Mh. Abbas Kandoro alitoa kauli kuwa kwa yeyote (mmiliki) wa magari ya abiria akigoma basi atafutiwa leseni ya biashara hiyo. Lakini pamoja na kauli hiyo kutolewa ya Mkuu wa mkoa bado baadhi ya watoa huduma hiyo wamekaidi agizo hilo na kusababisha usumbufu mkubwa wa usafiri kwa baadhi ya maeneo ikiwemo Kawe, Mwenge, Mtoni mtongani na kwingineko. Matokeo hayo ambayo yanasababishwa na bei ya mafuta, yanasababishwa na bei ya petroli mbichi (ambayo hupatikana huko kwenye mitambo) kupanda mpaka kufikia $160 na zaidi - kwa pipa moja. Kutokana na hali hiyo ambayo imeikumba nchi nyingi duniani, ni hali ambayo haipo katika uwezo wa mamlaka. Kwa kupata mbinu za kubana matumizi yako ya petroli bonyeza hapa
|
||||||||
|
Custom Search
|
||||||||
|
|
|
|||||||
|
©
www.zenjydar.co.uk - Since 2007 |
|
||||||||