Mount Kilimanjaro

 

 

 

Your community website

Beit El Ajaib
     

HomeNewsServicesEventsAbout UsContact Us

ProfileToolsGamesCommunity

NEWS

 
 

MAXIMO aongezewa mkataba

19/06/2008

Kocha wa timu ya taifa ‘Taifa Stars’ Marcio Maximo (Pichani) ameongezwa mkataba na Shirikisho la soka Tanzania (TFF) baada ya kuridhika na kazi aliyoanza kuifanya ambayo imeipandisha chati Tanzania katika medani ya soka.


Rais wa TFF, Leodegar Tenga alisema hayo jana jijini Dar mwezi mmoja kabla ya kumalizika kwa mkataba wa kocha huyo wa miaka miwili. Mkataba wa miaka miwili aliosaini kocha huyo kutoka Brazil utamalizika mapema mwezi ujao.“ Maximo aliingia mkataba nasi wa miaka miwili kuanzia Julai 28, 2006 hivyo mkataba wake huo utakamilika Julai 2,mwaka huu hivyo tumeona ni vema tulizungumzie jambo hili mapema na tumeamua kumwongezea mkataba huo kwa miaka miwili mingine” alisema Tenga.



Hata hivyo Tenga alisema pamoja na TFF kuamua kumwongeza mkataba wa kwa miaka miwili mingine na Kocha Maximo katika mazungumzo yao juu ya kuongezwa mkataba huo ameomba uongezewe mwaka mmoja tu kutokana na sababu zake binafsi ambazo hakuzitaja.

Akizungumza mara baada ya Tenga kutangaza uamuzi wa TFF kumwongezea mkataba wa kuinoa Stars, Maximo alisema sababu kubwa ya kufurahia jambo hilo na kushukuru kwa ushirikiano aliopewa kutekeleza majukumu yake na kueleza kuwa sababu yake ya kuomba apewe mwaka mmoja tu katika mkataba mpya ni kutoa nafasi kwa makocha wengine kuendeleza pale alipofikia katika programu ya kuinua na kuendeleza soka la Tanzania.


“Unajua mtu huwezi kutekeleza programu ya miaka 10 ya kuinua na kuendeleza soka la nchi pekee yako kwani kila programu ya kocha ina muda wake wa kukamilika hivyo katika mikaka hiyo 10 kuna ulazima wa kocha mwingine kuja kuendeleza pale nilipofikia” alisema Maximo.

Maximo aliiwezesha timu ya Taifa Stars katika mechi ya juzi kutoka 0-0 na timu ya Cameroon katika kuitafuta tiketi ya kwenda kushiriki kombe la dunia 2010 Afrika ya Kusini.

 

   
 

Custom Search

Go up

 

Quick Links

Watch Television
Events Calendar
News Archive 2008
News Archive 2007

External Links

Alnoor CET
TZ Embassy UK
TZ's Community UK

© www.zenjydar.co.uk - Since 2007 | Web master | Site map | www.zenjydar.co.uk - Since 2007 ©