Mount Kilimanjaro

 

 

 

Your community website

Beit El Ajaib
     

HomeNewsServicesEventsAbout UsContact Us

ProfileToolsGamesCommunity

NEWS

 
 

Jengo laporomoka - Dar es Salaam

21/06/2008

Leo hii jengo moja lililopo makutano ya mtaa wa Zanaki/kisutu limeporomoka kwa kile kinachohisiwa kuwa ujenzi usio makini. Inasemekana jengo hilo ambalo bado lilikuwa likiendelea na ujenzi lilikuwa limeshafikia ghorofa kumi kabla ya kuporomoka lote.

Habari ambazo bado hazijathibitishwa wakati uchunguzi ukiendelea zinasema kuwa baadhi ya mafundi waliokuwa wanalijenga jengo hilo ambao bado idadi yake haijajulikana wamefukiwa na hicho kifusi.

Wapita njia wakiwa karibu na eneo ambako jengo la ghorofa kumi lililokuwa linajengwa lilipobomoka lote leo.

Watu wanne wameopolewa na kukimbizwa hospitali. Habari za awali ambazo hazijathibitishwa bado zinasema wanasadikiwa kufa baada ya kufunikwa na kifusi cha jengo hilo.

Inasemekana watu hao wanne walikuwa ndani ya nyumba ya ghorofa tatu iliyo jirani na hilo ghorofa, ambapo baada ya kuangukiwa na kifusi wakawa wamenasa ndani.

Hadi milango ya saa kumi watu watatu walikuwa wameshatolewa, na juhudi za kumpata aliyesalia ama waliosalia zinaendelea. Pichani juu, Mwanazimamoto akijaribu kuangalia dalili za majeruhi.

 

   
 

Custom Search

Go up

 

Quick Links

Watch Television
Events Calendar
News Archive 2008
News Archive 2007

External Links

Alnoor CET
TZ Embassy UK
TZ's Community UK

© www.zenjydar.co.uk - Since 2007 | Web master | Site map | www.zenjydar.co.uk - Since 2007 ©