Mount Kilimanjaro

Beit El Ajaib
     

HomeNewsServicesEventsAbout UsContact Us

 
ProfileToolsGamesCommunity

NEWS

 
 

 

Zenjydar Community Association

01/05/2008

Tungependa kwa mara nyingine tena kutumia njia hii ya mawasiliano ili habari na ujumbe uweze kuwafikia jamii. Katika ujumbe huu Zenjydar Community Association itaelezea mambo yafuatayo kwa pamoja:

1.     Forum ya jumuia za East London

2.     Sherehe za Zenjydar kutimiza mwaka mmoja tangu iundwe

Zenjydar imezinduliwa rasmi KIKATIBA na kamati yake mwezi wa Mei mwaka 2007. Dhumuni kubwa ya kuundwa Zenjydar ni kuwa na chombo cha jamii cha kutoa huduma kwa kuangalia nini mahitaji ya wengi katika jamii ya Waswahili wa East London ambapo ni makao ya Zenjydar, na kutafuta njia za kuleta maendeleo katika mahitaji hayo iwapo mahitaji hayo yanafanana na yale tunayoyaafiki ambayo hayaleti utata au mpasuko katika jamii ya Watanzania na jamii ya Waswahili wa Afrika Mashariki na jamii zingine kwa ujumla kwa kushirikiana na jumuia zilizo karibu.

Kwa kuona kuwa, kuna mapengo makubwa ya huduma ambazo jamii zinahitaji, Zenjydar ikaamua kulenga katika matatizo makubwa ambayo jamii yetu inawarudisha nyuma kimaendeleo. Malengo hayo yamegusia kwenye Uajira, Elimu na mafunzo, Uendelezaji wa kazi za ustadi, kutoa ushauri kwa jamii katika mambo ya Uhamiaji (ikiwemo upataji wa sheria ya kuishi nchini UK), Nyumba, Afya na ustawi wa jamii kwa ujumla, na maendeleo ya Watoto na Vijana katika jamii ambayo hivi sasa tunaona ni ajenda kubwa kutokana na tunavyoona watoto na vijana wetu wanavyopotea katika jamii kuwa na anti-social behaviour (utovu wa nidhamu), crime (jinai), na matatizo ya kielimu.

Katika uchunguzi wetu, wengi wetu katika jamii ambao ukiangalia kundi kubwa la watu hawa katika jamii ni watu wenye ujuzi mkubwa wa kuchangia katika jamii yao kwa njia moja au nyingine lakini wanarudishwa nyuma katika maendeleo yao, maendeleo ya kuchangia jamii yao na maendeleo ya kuchangia taifa la UK na hata kuchangia nyumbani Tanzania, ni kwasababu ya ‘status’ yao ya makazi ya hapa nchini.

Baada ya Zenjydar kuanzishwa na kuanza kufanya uchunguzi (survey) ya wapi pa kuanzia kutatua matatizo hayo katika jamii, Zenjydar iliona kuna umuhimu mkubwa kukutana jumuia za Waswahili wa East London ambazo zinajihusisha moja kwa moja katika jamii. Baada ya mawasiliano mengi ya kufanya miadi ya mkutano na jumuia, East African Education Foundation ndio ilikuwa jumuia ya kwanza iliitika mwito na kufanya mkutano huo tarehe 12/08/2007. Baada ya mazungumzo marefu katika mkutano huo, Zenjydar ilikuja na rai ya kuanzisha ‘forum’ ya umoja wa jumuia hizi kwa madhumuni ya kuwa kitu kimoja ili tuweze kusaidia jamii. Jamii ambayo kihistoria imevunjwa nguvu kwa kutokana na mpasuko wa jumuia zilizopo awali.

Zenjydar inaamini, ikiwa jumuia zote zitakuwa na umoja wa kutekeleza jambo la kusaidia jamii kuhusu matatizo yanayokabili jamii, basi tunaweza kufika mbali kama walivyofikia jamii wa kutoka mataifa mingine ambao wanaishi katika nchi hii ya UK au nchi nyingine yoyote ile ughaibuni; na hasa ukiangalia nchi kama UK ambayo inatoa huduma nzuri kwa watu wake kielimu na vilevile ni nchi yenye sera ya ‘equal opportunities’ kwa kila mtu kuweza kuendelea.

East London Forum:

Baada ya mawasiliano mengi na kipindi kirefu kupita tangu mkutano wa kwanza wa Zenjydar na EAEF kufanyika, tarehe 01/01/2008 ukaitwa mkutano wa hafla wa jumuia kuja kuzungumzia ushirikiano wa kuleta maendeleo ya jamii. Jumuia husika zilikuwa ni Zenjydar Community Association, East African Education Foundation, Alnoor CET na Muzdalifah. Katika kikao hicho mambo mengi yalizungumzwa na nia ni kuwa jumuia zote ziwe na umoja kwa kuleta maendeleo katika jamii.

Vilevile kuna mengine ambayo yalijitokeza kutokana na yaliyopita ambayo yalileta mpasuko wa jumuia zilizopo awali kutokuwa pamoja hapo mwanzo na hili si la kufichika kwani hata jamii inafahamu. Lakini mwishowe katika mkutano huo jumuia zote nne ikiwemo Zenjydar zilifikia muwafaka wa kuunda kitu kimoja na kufanya mambo yao pamoja si kwasababu nyingine yeyote bali kusaidia na kuleta maendeleo katika jamii. Kwahivyo ikaamuliwa kuwa mikutano iwe kila mwezi mara moja na kila mkutano wa kila mwezi utasimamiwa au utashikwa kiti na jumuia husika kama duru; yaani ikiwa mwezi wa kwanza umesimamiwa na kushikwa kiti na East African Education basi mkutano ufuatao utasimamiwa na kushikwa kiti na jumuia nyingine na kuendelea hivyo hivyo na kujirudia tena.

Mwishowe maamuzi ya mkutano huo yalikuwa kuipa ‘priority’ au kipaumbele mambo matatu ambayo yalikuwa ni:

1.     Ujenzi wa msikiti;

2.     Kushughulikia mambo ya Maziko; na

3.     Elimu.

Ujenzi wa msikiti:

Katika jambo la ujenzi wa msikiti, jumuia ya Alnoor CET mpaka hivi sasa wamefika mbali na mradi wa kujenga msikiti ambao wanaita ‘The Masjid Project’. Kufika mbali ni kuwa tayari wana ‘policy’ ya msikiti huo, wana ‘plan’ ya mradi mzima wa msikiti huo, wana matangazo makubwa makubwa mpaka kwenye mtandao wao, na wameshangisha pesa kutoka katika jamii ambazo pesa hizo mpaka hivi sasa hazijafikia kiwango kinachotakikana cha kupata kununua jengo na kumaliza ujenzi wa msikiti mzima.

Halikadhalika, East African Education Foundation pia wana mradi wa ujenzi wa msikiti ambao pia wamekuwa nao tangu ya hapo awali lakini kutokana na mpasuko imeshindikana kufikia malengo mpaka hivi sasa ambapo wameamua tena kulifanya hili jambo la mradi wa msikiti.

Alnoor: wameamua kujenga msikiti Barking & Dagenham kwasababu masafa makubwa ya maeneo ya Barking & Dagenham hayana msikiti na nia yao ni kujenga msikiti ambao utakuwa na ‘access’ ya Waislamu wote.

East African Education Foundation: awali kabisa waliamua kujenga msikiti wa Waislamu popote pale East London ambao utasimamiwa na kuendeshwa na Waswahili kama misikiti ya Mungu ya jamii zingine za Kiislamu zilizopo East London.

Na jumuia zote mbili zina nia nzuri katika kufanikisha jambo hilo.

Mkutano wa tarehe 03/02/2008 ambao ulisimamiwa na Alnoor CET, ajenda ilikuwa ni ujenzi wa msikiti. Alnoor CET walipendekeza mradi wao wa msikiti kwa nia ya kutaka kushirikiana na jumuia zingine kufanya mradi huu kwa pamoja. Jumuia zingine zikaomba Alnoor walete sera au ‘policy’ ya mradi wa msikiti katika mkutano ufuatao kwa kuangalia vipi tutaweza kushirikiana katika jambo hilo.

Mkutano wa tarehe 02/03/2008 ambao ulisimamiwa na Zenjydar Community Association, sera za ujenzi wa msikiti zililetwa. Mwisho wa mkutano huo ilionekana kuwa sera ya ujenzi wa msikiti umeingiliana kiundani kabisa na katiba ya Alnoor ambayo ingesababisha Alnoor kubadilisha katiba na sera ili zilingane na kuzihusisha jumuia zingine husika katika mradi huo. Mwishowe iliamuliwa itakuwa si jambo la kuleta picha nzuri kwa jamii iwapo tutalikatia kabisa hili jambo kwasababu ya katiba au sera ya mradi wa msikiti. Kwahivyo ikaamuliwa mkutano wa tarehe 06/04/2008 jumuia zote zije na mapendekezo ya vipi tutaweza kuchangia katika mradi wa ‘The Masjid Project’ na vilevile kama kuna mapendekezo yoyote mapya kuhusu ujenzi wa msikiti. Mbali na hilo, vilevile East African Education Foundation walikuwa wameshaanza kuchangisha pesa za mradi wa msikiti mbali na ule wa Alnoor, kwa hivyo pia walipata fursa ya kuzungumzia hapo hapo mradi huo ambao upo katika awamu ya kwanza na nini lengo na madhumuni yake. Kwa kufanya hivyo, jumuia zote mbili si kama zimejigawa, bali rai hii ya ujenzi wa msikiti jumuia zote mbili zilikuwa nazo kabla ya umoja huu wa sasa ya jumuia zote hizi nne. Kwahivyo, hakuna jumuia ya kulaumiwa au ya kusema kuwa jumuia moja imejitenga na jumuia nyingine.

Mkutano wa tarehe 06/04/2008 jumuia zote zilikuja na mapendekezo ya vipi tutaweza kusaidia kuhusu mada hiyo ya ujenzi wa msikiti ‘The Masjid Project’ ya Alnoor.

Muzdalifah: wameafik rai ya ujenzi wa msikiti wa Alnoor na watasaidia kwa lolote watakaloombwa kusaidia lakini hawatokuwa na masuulia yoyote juu ya uongozi wa ujenzi wa msikiti kutokana na sera na katiba ya Alnoor ilivyofungamana (kufungamana kwa sera na katiba hiyo si kwa nia yoyote mbaya na zimeundwa kabla ya umoja huu). Muzdalifah imesisitiza kuipa kipaumbele jambo la Maziko.

EAEF: wameafik rai ya ujenzi wa msikiti wa Alnoor na watasaidia kwa lolote watakaloombwa kusaidia lakini hawatokuwa na masuulia yoyote juu ya uongozi wa ujenzi wa msikiti kutokana na sera na katiba ya Alnoor ilivyofungamana (kufungamana kwa sera na katiba hiyo si kwa nia yoyote mbaya na zimeundwa kabla ya umoja huu). EAEF imesisitiza kuipa kipaumbele jambo la mradi wa msikiti ambao wana mtazamo wa kushirikisha jumuia zote husika katika kufanikisha jambo hili. Mradi huo upo kipindi kirefu lakini hawajautangaza rasmi.

Zenjydar: wameafik rai ya ujenzi wa msikiti wa Alnoor na watasaidia kwa lolote watakaloombwa kusaidia lakini hawatokuwa na masuulia yoyote juu ya uongozi wa ujenzi wa msikiti kutokana na sera na katiba ya Alnoor ilivyofungamana (kufungamana kwa sera na katiba hiyo si kwa nia yoyote mbaya na zimeundwa kabla ya umoja huu). Zenjydar imesisitiza kuipa kipaumbele jambo la huduma za jamii kwa ujumla.

Baada ya mkutano huo wa mwisho, jumuia ziliondoka na suala moja tu la maziko ambalo limetiliwa mkazo sana na jumuia ya Muzdalifah na mkutano ufuatao umeamuliwa kuwa mwezi wa saba (July 2008).

Tarehe 19/04/2008 EAEF wametangaza katika Maulid yaliyotokea East London ya ujenzi wa msikiti na kutoa karatasi kwa jamii za mchango wa msikiti.

Kutokana na uchunguzi wa Zenjydar, imeonekana kuwa miradi hii ya ujenzi haitokuwa bila ya kuwahusisha jamii (community) ambao jumuia hizi zinategemea kila mtu kwenye jamii kuchangia kwenye miradi hii na sababu kubwa ambayo imejitokeza ya kupunguza kasi ya kufanikisha ujenzi wa msikiti na mengineyo ni kuwa jamii imeachwa njia panda bila ya kujua viongozi wanafanya nini na wamefikia uamuzi gani wa kufanikisha hili jambo na kwanini kuwe na miradi miwili badala ya kuwa na mradi mmoja halafu kuangalia mradi wa pili.

Katika mkutano wa tarehe 03/02/2008 Zenjydar ilipendekeza kuwa Waswahili wote waitwe kwenye muwaliko mmoja na viongozi wote wawepo kwenye mkutano huo waonyeshe umoja wao na waonyeshe kuwa hakuna mpasuko wowote kati ya jumuia hizi. Pendekezo hilo Zenjydar limeona linalega-lega na hasa mpaka uamuzi wa mkutano wa mwisho kuona kuwa jumuia zote zinajigawa tena kwenye makundi na kuamua kuweka vipindi virefu vya mikutano bila ya kuangalia uzito wa mambo yaliyopo katika jamii yakiwamo mambo hayo ya ujenzi wa msikiti na watoto.

Vilevile Zenjydar katika ‘experience’ yake ya mikutano yote iliyotokea na tunaamini na baadhi ya jumuia zingine vilevile wanamtazamo sawa na Zenjydar ya kuwa katika baadhi ya mikutano iliyopita kuna mambo yalijitokeza ambayo yalikuwa si mazuri na yalikuwa si ya kupendeza kwa watu wanaokaa kwa kufanya jambo lao kwa pamoja. Na hasa ikiwa watu kukaa pamoja kwa kuleta mambo yao binafsi ya mambo yaliyopita. Na haya vilevile yamesababisha chanzo cha kupunguza kasi ya umoja wa jumuia hizi badala ya KUJENGA ambalo ndio lilikuwa dhumuni kubwa ambalo limekusudiwa kukutana kwa jumuia hizi kuwa pamoja ili kufanya mambo yao kwa pamoja kwa kuleta maendeleo katika jamii.

Sherehe za Zenjydar kutimiza mwaka mmoja tangu iundwe:

Mwezi huu wa tano wa mwaka 2008, Zenjydar inatimiza mwaka mmoja tangu iundwe mwaka 2007. Dhumuni kubwa ya kuundwa kwa Zenjydar ni Kama tulivyosema mwanzoni hapo juu kuwa, Zenjydar ni chombo cha jamii cha kutoa huduma kwa kuangalia nini mahitaji ya wengi katika jamii ya Waswahili wa East London (ambapo ni makao ya Zenjydar) na kutafuta njia za kuleta maendeleo katika mahitaji hayo iwapo mahitaji hayo yanafanana na yale tunayoyaafiki ambayo hayaleti utata au mpasuko katika jamii ya Watanzania na jamii ya Waswahili wa Afrika Mashariki na jamii zingine kwa ujumla kwa kushirikiana na jumuia zilizo karibu.

Zenjydar imefikiria vya kutosha jinsi gani tutasheherekea sherehe za kutimiza mwaka mmoja tangu ianzishwe, kwanza kabisa kamati ilikuwa na rai ya kufanya Qasida ya kuita watoto wa chuo kwasababu zilizowazi kuwa (tunaangalia mahitaji ya wengi katika jamii ya Waswahili waliopo East London na jumuia tunazoshirikiana nazo) na tulikuwa tumeshaanza njia za kulifuatilia jambo hili. Lakini baada ya Kutokana na jinsi mambo mengi yanavyokwenda na yalivyojitokeza hapa katikati katika umoja wa ‘forum’ iliyokusudiwa dhumuni lake, Zenjydar imetumia HIKMA ya kubadilisha rai ya kufanya Qasida na kuamua kufanya Taarab. Rai hiyo ilikuwa hikma zake ni kama zifuatazo:

·          Zenjydar ilitegemea na iliona mbali kuwa kufanya hivyo, lazima baadhi ya watu watakuwa na hamu ya kujua msimamo wetu upo wapi katika umoja huu ambao unalegalega.

·          kutoa ujumbe kuwa kuna kazi kubwa ya kufanyika katika jamii kwa kukusudia kuwa, wapo watu ambao wamekuwa ‘ignored’ katika ‘community’ ambao huduma, habari na msaada kwao haufiki kama watoto na vijana na kwa wale ambao hawajihusishi na mambo kama ya Maulid au Qasida lazima kuwe na njia nyingine za kuwafikia ujumbe na kuweza kuwahusisha katika harakati za kijamii ili waweze kuchangia katika jamii yao.

·          kutoa ujumbe kuwa yaangaliwe madhara au athari ya jamii kwa kufanya ‘risk assessment’ ya jambo kuliko kuamua jambo kwa kutumia uamuzi wa wengi na kufunga masikio na kufunga macho na kudharau au ku ‘ignore’ watu walio wachache ambao pia wanatoka sehemu moja.

Baada ya kufikia uamuzi wa kufanya Taarab, Zenjydar ikatuma barua pepe kwa jumuia zote husika kualika katika sherehe hizo kabla haijaanza kutangaza dhahiri. Baada ya siku kadhaa kupita na majibu kutopatikana, Zenjydar ikaamua kuendelea na kukodi jumba la sherehe na kuanza kutangaza tukio la sherehe hizo katika jamii kwa njia ya mdomo tu.

Kutokana na kuwa siku zilikuwa hakuna tena, Zenjydar ikaendelea na mikakati ya tukio hilo. Na ‘Action Plan’ ya tukio ilikuwa liwe tukio la kiheshima, la kifamilia, kiingilio ni bure, zitengenezwe kadi za muwaliko ili kuwe na ‘control’ ya watu mlangoni, kuwe na mlinzi wa kukodi wa kuangalia kadi na watu, na itolewe dhifa na vinywaji vitamu.

Ilipofika tarehe 29/04/2008, Zenjydar ikapokea simu ya mkutano wa dharura kutoka kwa jumuia husika ambazo zilitaka kufanya kikao kuhusu muwaliko huo. Mwenyekiti wa Zenjydar akakaribisha kikao hicho na akasisitiza mkutano kufanywa siku hiyo hiyo saa 2 usiku (GMT) kwa mwenyekiti wa Zenjydar.

Uongozi wa juu kabisa wa jumuia zote ulifika katika mkutano huo ambao ulikuwa wa watu saba wa kutoka jumuia zote husika kati ya hao wawili kutoka Zenjydar.

Ulikuwa ni mkutano wa kijamaa na kirafiki na vilevile ulikuwa ni mkutano wa viongozi ambao wanajua nini msimamo wao. Kulikuwa hakuna ‘pressure’ wala ‘tension’ yoyote kwa upande wowote kwa waliohudhuria. Zenjydar ikaeleza kwanini imefikiria kufanya tukio hilo kwasababu zilizopo hapo juu na vilevile ikasisitiza jumuia kuwa na umoja bila ya kufarakiana katika malengo ya jamii. Kwani si Zenjydar tu, hata jamii wakiona viongozi au jumuia zinafarakiana wao pia wanausemi wa kusema “if you can’t understand me, how can you teach me”.

Mwenyekiti wa Zenjydar aliweka wazi kwanini kafikia ‘executive decision’ ya kutumia hikma ya uamuzi wa kufanya taarab na baadhi ya sababu za hikma yake zipo hapo juu na vilevile ilikuwa ni njia mojawapo ya ku ‘raise awareness’ kutokana na jinsi mambo yanavyokwenda katika umoja huu.

Zenjydar imesisitiza jumuia kushikana tena kuwa ‘serious’ na kuwa na umoja wa kuleta maendeleo ya jamii. Ama mtazamo wa Zenjydar kuhusu taarab ni kuwa, Zenjydar inachukulia taarab ni chombo cha utamaduni wa Tanzania. Mwenyekiti wa Zenjydar alisema nia yake kubwa ilikuwa ujumbe wake ufike kwa njia moja au nyingine.

Kamati ya Zenjydar imefikia uamuzi wa mwisho kufanya sherehe zake za kutimiza mwaka mmoja tangu iundwe kwa nia ya kuwa pamoja na jumuia zingine za karibu na kufanya jamii iwe pamoja nao. Zenjydar imeamua na kamati yake kufanya Qasida na kuzikaribisha jumuia zingine za karibu kuwa pamoja katika kuleta maendeleo ya jamii na wote waalikwa wanakaribishwa katika sherehe ya Zenjydar kutimiza mwaka mmoja.

Utamaduni wa Taarab:

Na kwanini taarab ni kitu cha utamaduni lakini kimefikia kubatilishwa katika jamii, je? Ni kwasababu inavyotumiwa siku za kileo kama ni chombo cha kuvutana na kushikana mashati na mpaka kubadilishwa jina kuitwa “Rusha Roho” badala ya kuitwa Taarab? Kwanini imefikia mpaka hata vyombo vya mamlaka kuanza kupiga vita zile nyimbo ambazo hazijengi jamii bali zinavunja jamii? Kwa maelezo zaidi ya kwanini taarab kupigwa vita bonyeza hapa

Baada ya yote haya na jahazi bado lipo safarini, tungependa kukumbushia tu katika wimbo wa filamu ya katuni ya Pocahontas ya Disney World ambayo inasema “You think the only people who are people are the people who look and think like you. But if you walk the footsteps of a stranger you’ll learn things you never knew, you never knew”.

 

       
 

Custom Search

Go up

Quick Links

Watch Television
Events Calendar
News Archive 2008
News Archive 2007

External Links

Alnoor CET
TZ Embassy UK
TZ's Community UK

© www.zenjydar.co.uk - Since 2007 | Web master | Site map | www.zenjydar.co.uk - Since 2007 ©