![]() |
Your community website |
![]() |
||||||
|
|
|
|||||||
|
|
||||||||
|
|
||||||||
|
|
||||||||
|
NEWS |
||||||||
|
|
||||||||
Akutwa na kichwa cha mtoto kwenye mfuko wa Rambo06/05/2008
Watuhumiwa Ramadhan Mussa na mama yake wakifikishwa mahakama ya Kisutu chini ya ulinzi mkali.
Ramadhan Mussa, kijana aliyekutwa akitafuna kichwa cha mtoto Salome Yohana, pamoja na mama yake mzazi Khadija Ali Selemani wamefikishwa mahakama ya Kisutu na kusomewa shitaka la mauaji. KICHWA cha mtoto kilichokamatwa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili kikiwa kimebebwa kwenye mfuko wa Rambo, kimezidi kuzua utata miongoni mwa jamii kutokana na tukio hilo lilivyotendeka. Wakazi wa jijini wamesema wamekumbwa na hofu kutokana na umri wa mtoto huyo Ramadhan Mussa (18), kushiriki kwenye vitendo hivyo vya ushirikina. Kufuatia tukio hilo wazazi wana hofu kuwa huenda matukio ya kupotea kwa watoto yanayoripotiwa mara kwa mara huambatana na vitendo hivyo vya ushirikina. Wakizungumza na magazeti tofauti kwa nyakati tofauti baadhi ya wazazi wameiomba Serikali kufuatilia kwa makini tukio hilo lililosisimua hisia za watu wengi na kutaka watuhumiwa wachukuliwe hatua kali za kisheria. Wameongeza kuwa huenda siku za mwisho zimekaribia kwani tangu karne hizo hawajawahi kutokea kuona mtoto wa miaka 18 akiwa anatembea na kichwa mitaani na kukitafuna hadharani. Mtoto Ramadhan alikamatwa mwishoni mwa wiki Hospitali ya Taifa Muhimbili na mlinzi Furgence Michael (38), akiwa na kichwa kilichosukwa nywele na baada ya kuhojiwa alidai anampelekea muuguzi mmoja wa hospitali hiyo zawadi. Kufuatilia tukio hilo wafanyakazi wa hospitali hiyo waliacha shughuli zao na kwenda kumshuhudia kijana huyo akitafuna kichwa hicho hadharani kwa madai kuwa amezoea kula nyama za watu na bibi yake iliwalazimu kumuweka chini ya ulinzi mkali. Baada ya polisi kufika walimuhoji mtoto huyo ambaye alidai kuwa alikuja na bibi yake anayeishi makaburi ya Jeti Lumo na kwa bahati mbaya wamemuacha na wao wamepaa na ungo. Kamanda wa Polisi Mkoa wa Ilala Kanda Maalum Dar es Salaam, Faustine Shilogile amesema kuwa hadi sasa wanawashikilia wazazi wa Ramadhan kujibu tuhuma hizo. Amesema kuwa mtoto Ramadhan amekuwa akipatikana kwenye matukio tofauti ya ajabu na wanaendelea kumchunguza kutokana na matukio hayo ili wabaini ukweli wake na hatua zaidi zichukuliwe juu yake. Tukio hilo limetokea Aprili 26 mwaka huu, saa 12 asubuhi, Segerea kwa bibi ambapo polisi wanawashikilia Ramadhan Musa, Lucas Kibaya ambaye ni baba wa kambo na mama yake Hadija Ally. Aprili 25 mwaka huu, Yohana Majani (26) na Upendo Datsun (27), wakazi wa Kimara wakiwa wameongozana na mtoto wao Salome Yohana (4), walikwenda kumtembelea shangazi yao Furaha Majani (28), anayeishi Segerea kwa Bibi. Ilipofika saa 2 usiku walibaini kuwa mtoto wao amepotea katika mazingira ya kutatanisha na walitoa taarifa kituo cha polisi baada ya kumtafuta kwa ndugu na jamaa bila mafanikio. Aprili 26 mwaka huu mtoto Ramadhan Mussa alikamatwa na kichwa cha mtoto huyo Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH), kikiwa kwenye mfuko wa Rambo akidai anampelekea zawadi muuguzi kwakuwa alimuhudumia vizuri hivi karibuni.
Baada ya wazazi kufika hospitali ya Muhimbili walitambua kichwa hicho ni cha mtoto wao. Kiwiliwili cha mtoto huyo na kichwa vimehifadhiwa Muhimbili. Leo hii Ramadhan na mama yake wamefikishwa mahakamani Kisutu, Dar es Salaam, kwa kushtakiwa na kesi ya mauaji.
|
||||||||
|
Custom Search
|
||||||||
|
|
|
|||||||
|
©
www.zenjydar.co.uk - Since 2007 |
|
||||||||