![]() |
Your community website |
![]() |
||||||
|
|
|
|||||||
|
|
||||||||
|
|
||||||||
|
|
||||||||
|
NEWS |
||||||||
|
|
||||||||
Safari ya barabara kuu kwenda majuu09/05/2008
Tumetumiwa picha na mwenzetu ambaye amependelea kuchangia stori yake ya safari yake ya kutoka London kuelekea mikoa ya juu. Pichani juu ni mwanamke asiyejulikana ambaye emesimama katika taa za barabara ya Finchley kwenda A406, London, akiwa na wenziwe wapatao 10 na vidoo vyao vya maji na wengine wakiwa na chupa za maji na sponji la kuoshea gari wakiwalazimisha watu wanaosimama kwenye taa hizo kuwapa pesa ili wawaoshee gari zao wakati wa kipindi wanachosimama kwenye taa. Iwapo utakataa kutoa pesa, wanaichafua gari yako kusudi kwa sponji kukuudhi tu! kama ionekanavyo hapo juu.
Lakini siyo yote ya kuudhi. Moto ni huduma ambazo zipo pembeni mwa barabara kuu za UK ambazo hutoa huduma za kuuza vitu reja reja, viburudisho na sehemu za kwenda haja; kwa kifupi ni sehemu ya mapumziko ambayo inakusaidia kutuliza kichwa kwa coffee au chai uwapo kwenye safari ndefu; Wanausalama wa barabara wanasisitiza kupumzika kwenye sehemu kama hizi katika safari yako kuepukana na ajali barabarani (picha imechukuliwa kwa ruhusa ya meneja).
Isitoshe, huduma ya kuvutia zaidi ya Moto ni huduma ya watoto kama uonavyo kwenye picha ambayo inaitwa motoBaby na nyingine motoKids. Usiwe na wasiwasi ukiwa na watoto kwenye safari yako au mtoto mchanga. Kitu cha kuvutia zaidi ni kuona kuwa kuna Warmer, Microwave, sehemu ya kumbadilishia mtoto na michezo ya kupumbaza watoto baada ya safari ndefu.
Watoto wana sehemu yao maalum ya kucheza na kujipumbaza na TV au kuchora vitabu.
Safari ya mikoani si mbali tena.
|
||||||||
|
Custom Search
|
||||||||
|
|
|
|||||||
|
©
www.zenjydar.co.uk - Since 2007 |
|
||||||||