Mount Kilimanjaro

 

 

 

Your community website

Beit El Ajaib
     

HomeNewsServicesEventsAbout UsContact Us

ProfileToolsGamesCommunity

NEWS

 
 

Plani mpya ya Queens Market yazinduliwa

14/05/2008

Pichani juu ni plani mpya ya soko kuu la Newham, Queens Market itakavyokuwa. Plani hiyo imetolewa baada ya kufanya uchunguzi wa kipindi kirefu cha mahitaji ya wakazi wa bara la Newham na vilevile ni moja ya kuendeleza mandhari ya bara la Newham likiwa kama ni bara ambalo Olympik ya London ya mwaka 2012 itakapofanyika.

Queens Market ni soko ambalo lipo Green street, East London, mtaa mmoja na uwanja wa mpira na klabu ya timu ya mpira wa miguu ya West Ham United (pichani).

Zaidi ya miaka 100, Queens Market imekuwa ikitoa huduma kwa wakazi wa bara la Newham na kwa umaarufu wake wa kupatikana na vitu vya kila aina kwa bei nafuu, limevutia wakazi wa kutoka mabara jirani ya Newham na hata wengine kutoka mikoani kufanya manunuzi yao ya kila mwezi kwenye soko hili.

Kwa kuwa Newham na isitoshe East London ni makazi ya watu wa kutoka mataifa mbalimbali duniani, linalifanya soko hili kuwa na bidhaa tofauti vya kutoka nchi za nje ikiwamo Afrika, Asia, Arabuni na bidhaa mbalimbali kutoka Marekani na hapa Ulaya.

Ndani ya Queens Market kuna maduka ya mapambo, vyakula (nyama ya ng'ombe, miguu, ulimi, utumbo, samaki, matunda na nafaka na vitafunio mbalimbali), hoteli za Halal, migahawa, bakery, maduka ya nguo, fanicha, vyombo na mapambo ya nyumbani na listi inaendelea...

Wakazi wengi wa kutoka sehemu tofauti za London na nje ya London husema nakuja Queens Market, Green Street, kwasababu nakuta vitu vyote ambavyo ninavihitaji. Wengine huita soko hilo "The world under one roof".

 

   
 

Custom Search

Go up

 

Quick Links

Watch Television
Events Calendar
News Archive 2008
News Archive 2007

External Links

Alnoor CET
TZ Embassy UK
TZ's Community UK

© www.zenjydar.co.uk - Since 2007 | Web master | Site map | www.zenjydar.co.uk - Since 2007 ©