![]() |
Your community website |
![]() |
||||||
|
|
|
|||||||
|
|
||||||||
|
|
||||||||
|
|
||||||||
|
NEWS |
||||||||
|
|
||||||||
Sherehe ya Zenjydar Community Association kutimiza mwaka mmoja17/05/2008
Mwenyekiti wa Zenjydar Community Association Bw. Saleh Jaber (pichani juu) akitoa zawadi ya fulana ya Zenjydar baada ya mvulana aliye pichani kujibu suali la mtego lililoulizwa hapo hadharani kwa waliohudhuria siku ya sherehe hiyo, huku Hafidh Karama wa EAEF (nyuma nyekundu) akiangalia tukio hilo. (Picha na Ali Muhidini). Zawadi hizo zilitolewa ikiwa kama ni moja ya harakati za sherehe hiyo ambayo si ya kutimiza mwaka mmoja kwa Zenjydar tu, bali ni mojawapo ya sherehe ya kujumuisha jamii. Mwenyekiti wa Zenjydar aliwashukuru wote waliohudhuria na aliwashukuru wote waliojitolea katika kufanikisha tukio hilo (wakiwamo Alnoor CET na EAEF na Muzdalifah) katika tukio ambalo vilevile lilijumuisha jamii ya Waswahili, East London. Alisema katika hotuba yake ambayo aligusia mambo tofauti, anafuraha kuona kuwa jumuia zote zinazosaidia jamii katika njia moja au nyingine zimejumuika na ameshauri umoja wa jumuia hizo uendelee ili kunufaisha jamii na kuinua ustawi wa jamii na mambo mbalimbali ambayo yanakuwa ni vigezo katika jamii ya Waswahili wa East London. Aliendelea na kusisitiza umuhimu wa kila mtu kwenye kuchangia nguvu kwenye jamii kwa kujihusisha na kujikurubisha katika sherehe kama hizi, mikutano na hafla za jamii yao pale wanapoitwa au wanapoalikwa ili waweze kuchangia sehemu mbalimbali katika maendeleo ya jamii na kushirikiana na jamii nyingine na jumuia nyingine ili kutanua mawazo ya kielimu na kiustadi. Si mara moja au mara mbili, mwenyekiti wa Zenjydar amesema jamii ya Waswahili wanauwezo wa kufanya lolote lile watakalolitaka la kuleta maendeleo yao ya kijamii iwapo watashirikiana pamoja popote pale walipo ughaibuni bila ya kuangalia tofauti zao, iwapo watakaa pamoja na kuangalia maeneo gani wataweza kushirikiana pamoja. Kwa kufanya hivyo, si kwa kujijengea wao tu, bali na watoto wao wa kizazi kipya kijacho. Iwapo watu watajigawa kimakundi, kuna hatari ya watoto kukulia upweke-upweke bila ya kuwa pamoja na jamii kubwa ya Waswahili itasambaratika ughaibuni bila ya kutambuana baada ya miaka 50 mpaka 100 ijayo na kupoteza utamaduni, mila na desturi yao. Mengi na kwa kifupi yalizungumzwa na mwenyekiti na mwisho wa hotuba aliwasihi waliohudhuria na jamii ya Waswahili kwa ujumla kuchangia nyumbani kwa kupitia mfumo wa Diaspora Skills Forum ili wachangie nchi yao na wapate wao wenyewe kufaidika. Vilevile mwenyekiti alirudia na kusema kuwa milango ya ubalozini ipo wazi na balozi yupo tayari kumsikiliza kila mtu anayetaka hoja yake kusaidiwa katika kuchangia nyumbani. Na kabla ya kufunga sherehe hiyo, mwenyekiti wa Zenjydar hakuwasahau wale waliochangia jumuia ya Zenjydar mpaka kufikia mwaka mmoja kwa kujitolea wakiwa kama 'Volunteers'. Aliwapatia shahada (certificate) za utambulisho na vilevile shahada mbili zilitolewa kwa Issa Mohammed na Salum (Muchacho) walituzwa na shahada ya kuwa watu wa kwanza kujiandikisha kujiendeleza kimasomo katika jamii kwa kupitia Zenjydar Community Association. Issa na Salum walitokea kuwa ni watu wa kwanza kabisa kujiandikisha kujiendeleza kimasomo kwa kupitia ZENJYDAR, mwenyekiti wa Zenjydar alisema, hiyo siyo miujiza, kuona kuwa Issa anatoka Zanzibar na Salum anatoka Dar es Salaam na ni watu wawili ambao wametoka njia tofauti hapa London bila ya kujuana na wametokea kuwa ni watu wa kwanza kujiandikisha kutumia huduma zetu; hiyo ni maana kamili ya ZENJYDAR COMMUNITY ASSOCIATION na amewasisitiza wengine wasisite wala wasione uzito kuuliza huduma gani zinapatikana kwa ajili yao. Picha za sherehe: bonyeza hapa kuangalia baadhi ya picha za sherehe. Iwapo utaona alama hii u utakapoweka mshale wa kubonyeza kwenye picha, bonyeza alama hiyo upate kuburudika na sura nzuri ya kuangalia picha hizo AU bonyeza sehemu ya chini kabisa ya picha hizo inayosema Start Slide Show. Ikiwa utabonyeza na haionyeshi kitu, itakubidi ku 'download' programu ambayo itakuomba u 'download'; fanya hivyo kisha burudika na picha.
|
||||||||
|
Custom Search
|
||||||||
|
|
|
|||||||
|
©
www.zenjydar.co.uk - Since 2007 |
|
||||||||