![]() |
Your community website |
![]() |
||||||
|
|
|
|||||||
|
|
||||||||
|
|
||||||||
|
|
||||||||
|
NEWS |
||||||||
|
|
||||||||
David Beckham kuupanda mlima wa Kilimanjaro19/05/2008
Mchezaji mpira wa miguu maarufu duniani David Beckham (33) amejiandaa kuupanda mlima mkubwa wa Afrika wa Kilimanjaro ambao upo Tanzania, katika mpango wa kujaza mfuko wa kusaidia watoto ambao umeandaliwa na UNICEF. Katika mpango huo, akiwa pamoja nae ni muimbaji mashuhuri BONO wa bendi ya muziki ya U2. Katika safari hiyo, BONO atakuwa akisaidia kujaza mfuko wa kusaidia watu wenye Ukimwi (HIV/AIDS).
Inasemekana kuwa, kutokana na urefu wa mlima wa Kilimanjaro ambao una urefu wa futi 19,340, kwa David Beckham itakuwa kazi si ndogo lakini kasema yeye mwenyewe kuwa atajitahidi kufika katika kilele cha mlima huo. Siku maalum bado haijapangwa kwasababu ya Beckham kuzingwa na kazi za timu yake ya Marekani, LA Galaxy. Inasemekana itawachukuwa siku 6 kuupanda mlima huo. Beckham kasema, kamchagua BONO kwenda nae kwenye safari hiyo kwasababu BONO ni mtu ambaye mwenye ushawishi mkubwa wa kumfanya yeye aupande mlima huo.
Vilevile, inasemekana golikipa wa timu ya West Ham United, Robert Green (pichani) atakuwa nao pamoja katika safari hiyo. Robert Green atakuwa akisaidia kujaza mfuko wa African Medical Research Foundation.
|
||||||||
|
Custom Search
|
||||||||
|
|
|
|||||||
|
©
www.zenjydar.co.uk - Since 2007 |
|
||||||||