![]() |
Your community website |
![]() |
||||||
|
|
|
|||||||
|
|
||||||||
|
|
||||||||
|
|
||||||||
|
NEWS |
||||||||
|
|
||||||||
Manchester United vs Chelsea ndani ya Urusi20/05/2008
Manchester United inapambana na Chelsea katika fainali ya kutafuta mshindi wa ligi ya European Cup 2008. Bila ya shaka, hili ni gemu kubwa ambalo linalongojewa na wengi wakiwemo wapenzi wa timu zote mbili (Manchester Utd. na Chelsea) na wengine wapenzi wa mpira wa miguu ambao hawatokubali kupitwa na gemu hili na kuacha kuwaangalia wachezaji wakubwa wa kimataifa. Mechi hiyo itafanyika kesho Jumatano ya tarehe 21/05/2008, katika uwanja wa Luzhniki huko Urusi wakati wababe hao wawili watakapovutana mashati na kupeperusha nyasi.
Je? Didier Drogba atapita kwa Rio Ferdinand? au Christiano Ronaldo atapita kwa Ashley Cole? au Wayne Rooney atapita kwa John Terry? yote hayo yanatukumbusha wakati wa upinzani wa miaka hiyo ya Simba na Yanga wakati wa Othman Juma Chama na Zamoyoni Mogella.
Kombe limeshafika Urusi kama lionekanavyo hapo juu kwenye uwanja wa Red Square. Mambo yote kesho Laivu kwenye ITV 1 na Sky Sports 1, saa 1 usiku mpaka mshindi apatikane.
|
||||||||
|
Custom Search
|
||||||||
|
|
|
|||||||
|
©
www.zenjydar.co.uk - Since 2007 |
|
||||||||