![]() |
Your community website |
![]() |
||||||
|
|
|
|||||||
|
|
||||||||
|
|
||||||||
|
|
||||||||
|
NEWS |
||||||||
|
|
||||||||
KARUME atoa maombolezo22/05/2008
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Amani Abeid Karume na mkewe Mama Shadya Karume wakisalimiana na Balozi Mdogo wa China anayeishi Zanzibar, LI,YIPING (katikati) pamoja na maofisa wengine walipofika Ofisi ya Ubalozi Mdogo Zanzibar kutia saini kitabu cha maombolezo kutokana na vifo vya maelfu ya wananchi wa nchi hiyo waliofariki kwa Tetemeko la Ardhi.
Mama Shadya Karume akisalimiana na balozi mdogo wa China anayeishi Zanzibar, LI,YIPING, wakati alipokwenda katika ofisi yake Mazizini kwa madhumuni ya kutia saini kitabu cha maombolezo ya vifo vya maelfu ya wananchi wa china waliofariki kutokana na tetemeko la ardhi lilitokea wiki iliyopita
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Amani Abeid Karume akitia saini kitabu cha maombolezo ya vifo vya maelfu ya wananchi wa China (waliofariki kutokana na tetemeko la ardhi wiki iliyopita) huko ofisi ya ubalozi mdogo Mazizini nje kidogo ya mji wa Zanzibar jana, Katikati ni mke wa Rais Mama Shadya Karume na Balozi Ndogo wa Chini Nchini LI,Yiping.
Mpaka leo hii namba ya watu waliokufa katika jimbo la Sichuan kutokana na metetemeko wa ardhi imefika 51,000 na watu 30,000 wamepotea au hawaonekani. Mamlaka ya jimbo la Sichuan wameomba tena matenti ya kukalia watu ambao wamepona yafikayo 3.3m.
Waliopona katika ajali hiyo ya mtetemeko wa ardhi, wamerejea katika makazi yao na kuangalia mabaki ambayo yanayoweza kutumika kuwasaidia katika siku zijazo ambazo hawajajua itachukuwa muda gani mpaka kupata makazi mapya. Mamlaka ya jimbo hilo wamesema, wameshaanza mpango wa kujenga mji mpya kilomita 20 kutoka mji uliokutwa na maafa. Mpango wa ujenzi wa mji mpya huo umethaminiwa kufikia kiwango cha £5bn.
Baada ya siku tatu za ukimya za maombolezo ya waliofikwa na maafa ya mtetemeko wa ardhi nchini China ambayo yamekwisha leo, na kabla ya miezi mitatu kufikia sherehe za Olimpik 2008 Beijing, mwenge wa Olimpik umeanza tena kukimbizwa kama kawaida katika jimbo la Zhejiang, China, na kesho Ijumaa kukimbizwa katika mitaa ya Shanghai na kuendelea katika miji mingine ya China mpaka kufikia kilele chake huko Beijing tarehe 08/08/2008 ambapo rasmi sherehe hizo za Olimpik zitakapoanza.
|
||||||||
|
Custom Search
|
||||||||
|
|
|
|||||||
|
©
www.zenjydar.co.uk - Since 2007 |
|
||||||||