Mount Kilimanjaro

 

 

 

Your community website

Beit El Ajaib
     

HomeNewsServicesEventsAbout UsContact Us

ProfileToolsGamesCommunity

NEWS

 
 

Semina ya (Drugs & Alcohol Awareness) - Zenjydar na DASL

25/05/2008

Dk. Mohammed Zahran MD. pichani kushoto akitoa semina kwa jamii iliyofanyika leo kuhusu madhara na athari ya kutumia vinywaji vikali na madawa ya kulevya kwa waliohudhuria katika semina hiyo ambayo imeandaliwa na Zenjydar Community Association ikishirikiana na Drugs and Alcohol Service for London (DASL).

Semina hiyo imekusudia kuelimisha jamii hasa vijana wanaoinukia wenye umri wa (teenagers) kupata kujua madhara ya vitu hivyo na vilevile kuelimisha wazazi kupata kutambua dalili za watoto wanapofikwa na janga hilo na njia za kuchukua kupata msaada ya jambo hilo.

Katibu Mkuu wa Zenjydar, Bw. Farid Nassor (pichani kushoto) na Hamid Kesi kulia wakijihudumia na vinywaji vyepesi na vitafunio wakati wa mapumziko ya semina hiyo ambayo ilianza saa 9 mchana mpaka saa 11 mchana.

Na baadhi ya watoto na vijana na wazazi waliohudhuria katika semina hyo wakijipatia vinywaji vyepesi na vitafunio wakati wa mapumziko.

Mwisho wa semina, Dk. Mohammed na mwenyekiti wa Zenjydar bwana Saleh Jaber walisisitiza umuhimu wa vijana kuhudhuria katika semina hizi na vilevile wazazi kujihusisha ili wapate kujua dalili, madhara na njia za kupambana na vitu hivyo. Vilevile Mbarak Hussein wa Alnoor alitoa fikra yake ya vitu kama hivi kufanyika mara kwa mara kuunganisha wazazi na watoto. Vilevile Ust. Gharib wa Muzdalifah alihudhuria katika semina hiyo.

Inatarajiwa semina hizi kufanyika tena siku za baadaye kwa jamii kwa ujumla.

 

 

   
 

Custom Search

Go up

 

Quick Links

Watch Television
Events Calendar
News Archive 2008
News Archive 2007

External Links

Alnoor CET
TZ Embassy UK
TZ's Community UK

© www.zenjydar.co.uk - Since 2007 | Web master | Site map | www.zenjydar.co.uk - Since 2007 ©