![]() |
Your community website |
![]() |
||||||
|
|
|
|||||||
|
|
||||||||
|
|
||||||||
|
|
||||||||
|
NEWS |
||||||||
|
|
||||||||
Bana matumizi ya Petroli27/05/2008
Kama tunavyojua kuwa petroli sasa imevuka mpaka bila ya kutegemea kwa kipindi kidogo tu na kuvuka £1.10 kwa lita moja na bei hiyo inazidi kupanda kila kukicha. Zenjydar, imejaribu kukusanya habari kutoka sehemu tofauti kutafuta njia za kukata matumizi yako ya petroli. Wiki iliyopita bei ya petroli mbichi (ambayo hupatikana huko kwenye mitambo) imefika $135.00 kwa pipa moja ambayo imesababisha kupanda kwa bei ya petroli kwa asilimia 40% mwaka huu peke yake. Hali hii imemkumba kila mtu ambaye anategemea usafiri wa gari na vilevile imekumba mashirika makubwa makubwa yanayotegemea mafuta yakiwemo mashirika ya ndege. Mashirika ya ndege yameonya, kutokana na hali hii, itawabidi wapunguze idadi ya ndege zinazosafiri na kuongeza bei ya usafiri wa ndege ili wabane matumizi kuepukana na kupigwa na hasara ya mashirika yao. Makampuni ya magari pia wameonya kuwa kuna hatari ya kupata hasara kwa kupungua kwa idadi ya wateja kuja kununua magari kutokana na hali inavyokwenda ambayo inategemewa baada ya wiki nne mpaka wiki sita zijazo bei ya mafuta itapanda tena kwa peni mbili unusu juu ya bei iliyopo hivi sasa. Kwahivyo, kaeni mkao wa kula. Lakini njia gani unaweza kuzichukua ambazo zitakusaidia kubana matumizi ya mafuta? TAFUTA TOFAUTI YA BEI: Kwanza kabisa, angalia eneo unalokaa kuna stesheni ngapi za petroli ambazo unazijua na kabla haujatia petroli zunguka stesheni zote za eneo lako kuangalia bei nafuu. Kwa kufanya hivi itakusaidia kubana pesa. Chini ya maelezo haya, tumekuwekea kubonyeza link ya mtandao wa kukuwezesha wewe kutia Post Code ya eneo lako kujua stesheni zote za karibu yako unapoishi na bei zake. Mtandao huo utakupa tofauti ya bei zote za stesheni za sehemu unayoishi (up to date) bei ghali na bei ya chini. Bei za kila eneo hutofautiana mpaka 15p kwa lita moja ambayo ikiwa unajaza tenki la petroli la lita 40 unaweza ukasevu mpaka £6.00. ENDESHA GARI KIMAKINIFU: Tumia muda mrefu kuendesha gari kwa kutumia gea ndogo (gea namba 5). Unapoondoa gari, usitumie muda mrefu kuvuta kwenye gea kubwa (gea namba 1, 2, 3 na 4) gea namba hizi hutumia mafuta mengi. Kwa kusema ukitumia gea namba 3 kwenye mwendo wa 37mph inakunywa asilimia 25% ya mafuta zaidi kuliko ukiwa unatumia gea namba 5 kwenye mwendo huo huo. Vilevile unapokwenda safari ya mbali au safari yenye magari mengi, pendelea kusikiliza habari za TRAFFIC za redioni za kwenye gari kama (BBC 94.9) ambayo huleta habari za TRAFFIC kila baada ya dakika 15. Kufanya hivi, kutakusaidia kuepukana na njia zenye magari mengi au njia iliyo na ajali ambayo itakusababisha wewe kukaa kwenye foleni ya magari kwa kipindi kirefu. TAFUTA NJIA TOFAUTI ZA USAFIRI: Jaribu kutafuta njia tofauti za usafiri ili kubana matumizi na kusevu matumizi ya petroli ya gari yako. Mfano, tafuta rafiki au mfanyakazi mwenzio ambaye mnafanya wote kazi pamoja kwenda kazini na gari moja lakini kuchangiana pesa za petroli badala ya wewe kulipa pesa zote peke yako. Jaribu kutumia usafiri wa umma kama (basi au treni) badala ya usafiri binafsi. Jaribu kutumia baiskeli ambayo itakusaidia kubana matumizi ya petroli na vilevile itakufanya uwe na afya nzuri. Vilevile inapendekezwa kama unafikiria kununua gari mpya, basi fikiria kununua "Green Car" ambazo zinatumia umeme au (Electric, Hybrid, Hydrogen and Solar cars). Kwa hapa UK, gari hizo zinasaidia kukata gharama ya TAX na vilevile inasaidia kukata gharama ya petroli. Inasemekana kuwa, robo ya magari ambayo yapo UK hutumiwa kutembelewa na safari zisizozidi maili 2 (2 miles) ambazo safari hizo zingeweza kutumiwa kwa njia ya mguu au (kutembea kwa mguu). Bonyeza mtandao ufuatao kuangalia bei za petroli zilizopo karibu na maeneo unayoishi:
|
||||||||
|
Custom Search
|
||||||||
|
|
|
|||||||
|
©
www.zenjydar.co.uk - Since 2007 |
|
||||||||