Mount Kilimanjaro

 

 

 

Your community website

Beit El Ajaib
     

HomeNewsServicesEventsAbout UsContact Us

ProfileToolsGamesCommunity

NEWS

 
 

Newham Football Tournament 2008 - Zenjydar Team

28/05/2008

Timu ya Zenjydar ya umri wa miaka 8 - 11, wameshiriki katika mashindano ya mpira wa miguu ambayo yameandaliwa na bara la Newham katika kutafuta mshindi wa Newham.

Vijana wa Zenjydar wamepigana vya kutosha katika mechi za mtoano kwa kuzifunga timu zingine zilizoshiriki na kufikia karibu na fainali, lakini hatimaye walitolewa na timu ambayo iliwazidi nguvu kidooogo.

Kocha wao Bw. Steve au (kwa jina lingine Farooq) alisema, amefurahika na vijana kwa jinsi walivyocheza na alitabiri kwa kusema kuwa, kama wangejuana kwa kipindi kirefu kwenye mazoezi basi wangeshinda semi fainali na kuingia fainali.

Halikadhalika, Vijana wa timu ya Zenjydar wa umri wa miaka 15 - 17, pia walifanya uzuri na kushindwa kwenye semi fainali kuelekea fainali.

Kama wangeshinda semi fainali, wangekwenda kuonyesha ustadi wao kwenye fainali ambayo itakuwa kwenye uwanja wa mpira wa miguu wa West Ham United, Green Street.

Wachezaji wote walipata zawadi ya medali ya kushiriki katika mashindano hayo.

Fainali itakuwa tarehe 30/05/2008, Ijumaa, West Ham United, Green Street, kuanzia saa 10 mpaka saa 3 usiku ambapo atapatikana mshindi.

 

   
 

Custom Search

Go up

 

Quick Links

Watch Television
Events Calendar
News Archive 2008
News Archive 2007

External Links

Alnoor CET
TZ Embassy UK
TZ's Community UK

© www.zenjydar.co.uk - Since 2007 | Web master | Site map | www.zenjydar.co.uk - Since 2007 ©