Wahanga wa Disko Toto
wazikwa - Tabora
09/10/2008

MJI wa Tabora uligubikwa
na simanzi na vilio miongoni mwa wazazi, walezi, ndugu na jamaa wakati
wakiitambua miili ya watoto 19 waliokufa katika kumbi za Disko za
Bubbles Night Club na Top Five Disco Sound mjini Tabora baada ya kukosa
hewa.
Miili ya watoto hao wenye
umri wa kati ya miaka saba na 18 ilianza kuzikwa leo katika makaburi
mbalimbali ya mjini Tabora, kwa kufuata imani zao za dini.
|