Baraza la Eid - London
2008
11/10/2008

Kutoka kushoto: Ustadh Makoe, Maalim
Abdallah (Mwenyekiti wa ZAWA), Idris Zahran (Ofisa wa habari na
mawasiliano Ubalozini UK), Mohammed Zahran (Katibu wa East African
Education), Saleh Jaber (Mwenyekiti wa Zenjydar Community Association),
Ustadh Issa, Ustadh Khamis Faki (Mwenyekiti msaidizi East African
Education Foundation), Salum Abdallah na wajumbe wengine waliohudhuria
katika hafla ya baraza la Eid London 2008.

Kutoka kushoto: Bwana Idris Zahran, Abuu
Faraj (Mwenyekiti TZUK Association), Saleh Jaber (Mwenyekiti Zenjydar
Community Association), Ustadh Nassor Haroub (Mwenyekiti East African
Education Foundation) na Abdallah Maka.

Habari Kamili:
Baadhi ya jumuia za East London
zilihudhuria kwenye baraza la Eid ambalo limefanyika tarehe 11/10/2008.
Baraza la Eid limeandaliwa na jumuia ya ZAWA ikishirikiana na East
African Education Foundation na TZUK Association na Ubalozi wa Tanzania
nchini UK.
Hii ni mara ya pili baraza la Eid
kufanyika tangu mwaka 2007 na kusimamiwa rasmi na Maalim Abdallah.
Katika hafla hiyo, mgeni wa heshima bwana
Idris Zahran ambaye aliwakilisha Ubalozi wa Tanzania nchini UK alipata
fursa ya kukaribisha wote waliohudhuria na kuleta salamu za Mheshimiwa
balozi Mwanaidi Maajar Sinare za Eid Mubarak.
Vilevile bwana Idris alisema, Mheshimiwa
balozi anaanzisha mpango wa kukutana na wote wenye jambo lolote ambalo
wangependelea kuongelea na Mheshimiwa katika kuleta maendeleo. Mpango
huo ambao utakuwa kila siku ya Alhamisi, itakuwa ni siku maalumu kwa
yoyote atakayependelea kukutana na mheshimiwa balozi Mwanaidi Maajar.
Picha na Ustadh Khalfan kwa niaba ya
Zenjydar Community Association.
|