Mount Kilimanjaro

Beit El Ajaib
     

HomeNewsServicesEventsAbout UsContact Us

 
ProfileToolsGamesCommunity

NEWS

 
 

Bara la NEWHAM kupambana na madereva hewa

12/10/2008

Bara la Newham ikishirikiana na Metropolitan Police wameunda kikosi cha kupambana na madereva hewa (madereva ambao wanaendesha gari bila ya Leseni au bila ya Bima (Insurance).

Kikosi hicho ambacho kinaitwa "Operation Reclaim" kimezinduliwa rasmi na Diwani Ian Corbett pamoja na Kamanda wa Polisi wa Newham, Simon Letchford, baada ya matayarisho yaliyoandaliwa katika kituo cha Polisi cha Forest Gate, Newham.

Operesheni hiyo itakuwa inakamata mitaani na barabarani magari na madereva ambao hawana Bima au Leseni.

Kamanda Letchford ametoa onyo kali akisema, "Operation Reclaim" ni nguvu ambayo inawapa Polisi kusimamisha magari ambayo hayana Bima kwa kutumia vyombo maalum ambavyo vimo ndani ya gari za Polisi. Mara tu gari itakapokamatwa baada ya kutambulika kuwa haina Bima, Polisi watamtoza dereva faini £300.00 hapo hapo kwa kumpa tiketi na kuchukuliwa gari yake hapo hapo.

Dereva anatakiwa akomboe gari yake kwa kulipa faini hiyo na kuonyesha Bima mpya ndani ya siku zisizozidi 14 baada ya tukio. Ikiwa siku 14 zitapita na gari haijakombolewa, gari hiyo itapondwa na mashine maalum au itauzwa kwenye mnada.

Operesheni hiyo iliwekwa kwenye majaribio mwezi wa tisa (Septemba) mwaka huu na Polisi walifanikiwa kukamata magari 336 ambayo hayana Bima (Insurance).

Polisi wamesema, wanaamini katika bara la Newham peke yake, hivi sasa kuna magari yasiyopungua 20,000 mpaka 30,000 ambayo hayana Bima.

 

   
 

Custom Search

Go up

 

Quick Links

Watch Television
News Archive

© www.zenjydar.co.uk - Since 2007 | Web master | Site map | www.zenjydar.co.uk - Since 2007 ©