007 Aston Martin, gari
bora ya mwaka 2008
13/10/2008

Gari maarufu ya Aston Martin DB5 ambayo
hutumiwa sana na 007 James Bond imeshinda na kuchaguliwa kuwa namba 1
kama ni gari bora ya mwaka 2008.

Aston Martin DB5 imetumiwa na James Bond
katika filamu yake mpya Quantum of Solace. DB5 ina nguvu ya lita 6,
injini V12 ambayo ina uwezo wa kusukuma 510bhp ambayo yenye spidi
200mph. Maana yake ina uwezo wa kufika 62mph kutoka 0mph kwa muda wa
sekunde 4.3

Gari iliyoshinda katika kundi la gari za
kifamilia ya mwaka 2008 ni Audi A4 kama ionekanavyo pichani juu ikiwa
katika maonyesho yake mjini Seoul, Korea ya Kusini.

Gari iliyoshinda katika kundi la gari
zenye miundo midogo ni gari mpya Fiat 500.

Gari iliyoshinda katika kundi la gari za
kifahari ya mwaka 2008 ni Jaguar XF Sedan kama ionekanavyo pichani juu.

Gari iliyoshinda katika kundi la magari
yenye nguvu ya matairi yote manne au (4x4) ni Ford Kuga kama ionekanavyo
pichani juu.

Gari iliyoshinda katika kundi la magari ya
Spoti au (Sports Car) ni Mitsubishi Evo X kama ionekanavyo pichani juu.
|