Mount Kilimanjaro

Beit El Ajaib
     

HomeNewsServicesEventsAbout UsContact Us

 
ProfileToolsGamesCommunity

NEWS

 
 

Wanne watiwa ndani kwa janga la Disko Toto Tabora

14/10/2008

Jengo lililokuwa na ukumbi wa Disco la Bubbles, uliosababisha maafa siku ya Eid ya kwanza ya Eid-el-fitr.

WATU wengine wawili wamekamatwa wakituhumiwa kuhusika na tukio lililosababisha vifo vya watoto 19 waliokufa wakati wanacheza muziki siku ya Eid Mosi.

Polisi imesema kuwa waliokamatwa ni Meneja wa disko la One Ten Teck, Jaffar Rashid na Meneja wa Bubbles Night Club, Vituko Salala.

Kabla ya kukamatwa kwa mameneja hao, Polisi waliwakamata wamiliki wa madisko hayo ambao ni Projestus Fidelis na Shashikant Manji Patel.

Kwa mujibu wa vyombo vya dola watu hao ndio waliandaa disko la watoto katika siku hiyo ya Eid-el-fitr. Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Abeid Mwinyimsa, alisema leo kuwa wakurugenzi hao na mameneja wanashikiliwa na polisi kwa ajili ya kuhojiwa kuhusu chanzo cha tatizo lililosababisha watoto hao kupoteza maisha.

Alisema Polisi imempa taarifa rasmi ya kushikiliwa kwa watu hao, huku ikimuarifu kwamba walinzi wa milangoni katika madisko hayo mawili "Mabaunsa" nao wanasakwa ili waweze kuhojiwa kuhusu sakata hilo. Mkuu huyo wa Mkoa alisema wakurugenzi hao, watahojiwa pia na Tume huru iliyoundwa kwa ajili ya kuchunguza mkasa huo, ambayo alisema imeshaanza kazi yake na kuwataka wananchi waipe ushirikiano ili iweze kupata taarifa za ukweli zitakazofanyiwa kazi na serikali.

Katika siku hiyo ya Eid, watoto 19 walikufa na wengine kulazwa hospitali ya mkoa ya Kitete baada ya kukosa hewa katika kumbi za disko wakati wakiwa katika sherehe ya Eid-el-fitr.

 

   
 

Custom Search

Go up

 

Quick Links

Watch Television
News Archive

© www.zenjydar.co.uk - Since 2007 | Web master | Site map | www.zenjydar.co.uk - Since 2007 ©