Madereva kusimamishwa
Udereva
15/10/2008

Kuzidi kwa idadi ya
magari na kuzidi kwa madereva hatari barabarani, wizara ya usalama wa
barabara wametangaza rasmi kuwa, dereva yoyote atakayepatwa na makosa
mawili atasimamishwa kuendesha gari.
Kosa la kwanza, mkosa
atapewa pointi sita katika leseni yake, kosa la pili atakuwa na pointi
kumi na mbili ambazo zinamfanya moja kwa moja kusimamishwa kuendesha
gari. Katika makosa makubwa moja wapo ni kosa la kwenda kasi na kupita
kiwango kinachoruhusiwa barabarani.
Waziri wa usalama wa
barabara bwana Jim Fitzpatrick amesema, hatua hii itatizama siyo wenye
kwenda mbio na magari na kuhatarisha usalama wa watu tu, vilevile sheria
hii itaangalia vikali kwa wale wenye kuendesha gari wakiwa wamelewa na
vilevile kwa mara ya kwanza sheria hii mpya itawakumba wale ambao
wanakula vidonge vya dawa kwa matibabu yao (kama homa, flu, kichwa na
kadhalika) lakini madawa hayo
yanawafanya wapitiwe na usingizi (Drowsy) na kuwafanya wasiweze kuwa
macho au kuwa makini katika kuendesha gari wanapokuwa barabarani.
|