Gari yapiga mbizi
Kivukoni - Dar es Salaam
18/10/2008

Askari wa kituo kidogo cha
feri wakila doria sehemu lilipotumbukia na kuzama gari aina ya Canter,
feri, kivukoni, huku MV Kigamboni ikila mzigo na kufanya safari zake za
Kigamboni na kurudi kama kawaida. Chini ni wapiga mbizi wakiwa katika
harakati za kulifunga kamba gari hilo.

Gari aina ya Canter limetumbukia baada ya
kushindwa kupandisha kimlima cha kutokea kwenye Pantoni upande wa Posta.
Hakuna mtu alilyedhurika na ajali hiyo.
Dereva ambaye alikuwa peke yake wakati akitoka kwenye Pantoni, aliamua
kuruka baada ya kuona gari imegoma kusimama licha ya kuweka kigogo na
utingo wake aliyekuwa nje ya gari.
Juhudi za kulitoa gari hilo katika maji
zilishughulikiwa ambapo Wazamiamaji walikuwa wakipiga mbizi kulifunga
kamba kabla ya kuliopoa. Inasemekana walifanikiwa kulitoa gari hilo kwa
usalama, lakini bado usalama wa kivukoni unahitaji mtazamo wa karibu
kwani inasemekana hali kama hizo kutokea si mara ya kwanza.
|