Mount Kilimanjaro

Beit El Ajaib
     

HomeNewsServicesEventsAbout UsContact Us

 
ProfileToolsGamesCommunity

NEWS

 
 

Kadi za wageni wanaoishi nchini UK

20/10/2008

Hatimaye, Serikali imezindua kadi mpya za wakazi au wageni ambao si raia wa UK ambao wanaishi nchini UK kwa madhumuni mbalimbali.

Kadi hizo ambazo zinaitwa "Biometric Cards" zitatolewa katika wimbi la kwanza katika mwezi wa kumi na moja Novemba 2008, kwa Wanafunzi ambao si raia wa UK lakini wanaishi nchini UK ambao pia si raia wa nchi zilizoungana za Ulaya (European Union) na zitatolewa kwa wale ambao wana Viza ya ndoa.

Waziri wa mambo ya ndani bi Jacqui Smith amesema, Kadi hizo zitasaidia kurahisisha kumtambua mwenye kadi kirahisi kuwa ni yeye anayemiliki kadi hiyo ambayo itakuwa na habari zote za mwenye kumiliki kadi ikiwamo hali yake ya makazi ya nchini UK.

Ameongeza akisema, kadi hizo zitasaidia wale ambao wamo nchini si kihalali kutambulika kirahisi popote watakapoenda na kutokufaidika na misaada (benefits) ambayo ni ya raia wa UK.

Kadi hiyo ambayo itatolewa badala ya karatasi na muhuri ambazo zilizokuwa zikitolewa hapo mwanzoni, zitakuwa na jina la mwenye kadi, picha yake, uraia wake, vipi anakaa nchini na alama ya vidole viwili (fingerprints).

 

   
 

Custom Search

Go up

 

Quick Links

Watch Television
News Archive

© www.zenjydar.co.uk - Since 2007 | Web master | Site map | www.zenjydar.co.uk - Since 2007 ©