Mount Kilimanjaro

Beit El Ajaib
     

HomeNewsServicesEventsAbout UsContact Us

 
ProfileToolsGamesCommunity

NEWS

 
 

Bakwata yashutumu mauaji ya Albino (Zeruzeru)

22/10/2008

Baraza Kuu la Waislamu wa Tanzania (BAKWATA), limesema linaunga mkono kauli ya Rais Jakaya Kikwete, kwamba watakaobainika kuwaua albino na watu wengine wachukuliwa hatua kali ili vitendo hivyo visijirudie tena nchini.

Akitoa tamko kwa waandishi wa habari Dar es Salaam jana, kwa niaba ya Sheikh Mkuu wa Tanzania, Mufti Issa bin Shaaban Simba, Kaimu Mufti, Sheikh Suleimani Gorogosi alisema hatua kali dhidi ya wauaji hao zinapaswa kuungwa mkono kwa asilimia 100.

Alisema siyo kazi ya rais pekee wala viongozi wa juu kukabiliana na vitendo hivyo vya kinyama, bali ni ya jamii nzima hivyo wao kama Bakwata wanapinga na kulaani unyama wanaofanyiwa albino. “Tunamuunga mkono rais kwamba hatua kali zichukuliwe dhidi ya wauaji hao maana kama hawatakomeshwa basi watahamia kwa walemavu wengine, vikongwe na watu wengine na hii italiondolea sifa taifa hili la amani duniani.” alisema Mufti Simba.

Alisema ni ujinga watu kudhani kuwa viungo vya albino vinaleta utajiri kwani hao ni binadamu kama wengine na hakuna uhusiano wowote wa utajiri na viungo vya binadamu, bali utajiri unapatikana kwa kufanya kazi kwa bidii na uaminifu. Katika hatua nyingine, Bakwata imewaagiza masheikh na maimamu katika misikiti yote nchini kutoa mawaidha ya kuwaelimisha waumini kuhusu maadili, na kulaani kitendo cha baadhi ya watu katika Kijiji cha Kanga, wilayani Chunya, Mbeya kupiga mawe magari yaliyokuwa katika msafara wa rais wiki iliyopita.

Zaidi ya maalbino 20 wameuawa katika maeneo mbalimbali nchini hasa mikoa ya Mwanza, Shinyanga, Kagera, Mbeya na Mara, na hadi sasa watu 47 wanashikiliwa na polisi wakihusishwa na mauaji hayo.

 

   
 

Custom Search

Go up

 

Quick Links

Watch Television
News Archive

© www.zenjydar.co.uk - Since 2007 | Web master | Site map | www.zenjydar.co.uk - Since 2007 ©