Mount Kilimanjaro

Beit El Ajaib
     

HomeNewsServicesEventsAbout UsContact Us

 
ProfileToolsGamesCommunity

NEWS

 
 

URAFIKI

23/10/2008

Balozi msaidizi wa Tanzania nchini UK, bwana Chabaka Kilumanga (kushoto) akipokea kwa tabasamu la bashasha sanaa ya picha ya kuchorwa inayogusia mila na utamaduni wa Tanzania kutoka kwa bwana Andrew Marshall, aliyekuwa Mkuu wa Mkoa (District Commissioner) wa Tarime mwaka 1948 wakati Tanzania ilipokuwa katika ukoloni wa Great Britain na ikijulikana kama (Tanganyika) miaka hiyo.

Picha hiyo tangu balozi wa kwanza nchini UK baada ya uhuru wa Tanganyika, bwana Sam Ntiro, ilitolewa rasmi kwa balozi msaidizi bwana Chabaka Kilumanga nyumbani kwa bwana Andrew Marshall mjini Bath, UK, Alhamisi iliyopita tarehe 16/10/2008

Bwana Kilumanga alitoa shukran za dhati kwa bwana Marshall, na kuahidi kuitundika picha hiyo ndani ya chumba kimoja wapo kilichopo ubalozini UK ili wageni wajapo waone uhusiano mkubwa wa kihistoria unaotoka mbali kati ya Tanzania na United Kingdom.

 

   
 

Custom Search

Go up

 

Quick Links

Watch Television
News Archive

© www.zenjydar.co.uk - Since 2007 | Web master | Site map | www.zenjydar.co.uk - Since 2007 ©