Mount Kilimanjaro

Beit El Ajaib
     

HomeNewsServicesEventsAbout UsContact Us

 
ProfileToolsGamesCommunity

NEWS

 
 

Ch. 4 yatafuta familia ya kucheza silisila ya "The Family"

25/10/2008

Channel 4 ya UK ipo katika harakati za kufanya silisila ya "The Family" kwa mara ya pili. Silisila hiyo inahusu maisha ya kweli ya watu au familia za Great Britain wanavyoishi maisha yao ya kweli nchini UK.

Firefly, ambao ni waendeshaji wa programu hiyo kwa niaba ya Channel 4, wametoa fursa kwa familia itakayopendelea kushiriki katika salasila hiyo wajitokeze ili waweze kuwa nao kwa kipindi cha miezi minne wakiwa katika kutengeneza salasila hiyo ya pili ya "The Family" ambayo yatagusia maisha ya familia hiyo wanavyoishi kikweli katika maisha yao ya kila siku.

Waendeshaji wa salasila hiyo wangependelea kuangalia mambo yoyote yanayogusia familia yoyote ambayo itajitokeza ya UK aidha kwenye mambo ambayo familia inatatizwa na kupata shule ya karibu na watoto wao wanapoishi, au watoto hawataki kwenda shule kwasababu ya uhuni na wazee wanajitahidi kuwapeleka shule, au kuhusu jambo lolote linalogusia maisha ya kila siku ya kifamilia (harusi, siku za kuzaliwa, na kadhalika).

Familia yoyote inaweza kushiriki bila ya kuangaliwa wapi wanatoka au rangi yao au taifa lao.

Channel 4 imesema, familia itakayobahatika kushiriki, itakuwa ni fursa kubwa katika maisha yao kuwamo kwenye filamu ya UK na familia yao nzima.

Kama ungependelea kujiandikisha, tuma barua pepe kwenye anuani ifuatayo, Email: family@fireflyproductions.tv ukiambatanisha na namba yako ya simu, anuani na maelezo mafupi juu ya familia yako, au kwa maelezo zaidi, piga simu 020 7033 2270.

 

   
 

Custom Search

Go up

 

Quick Links

Watch Television
News Archive

© www.zenjydar.co.uk - Since 2007 | Web master | Site map | www.zenjydar.co.uk - Since 2007 ©