Yanga yaicharaza
Simba 1-0
26/10/2008

Mchezaji wa Yanga Ben Mwalala akipachika
bao wavuni huku kipa wa Simba Amani Simba akiuangalia bila kufanya
lolote katika mchezo wa Ligi Kuu uliofanyika leo jijini Dar es Salaam.
Matokeo ya mechi hiyo: YANGA 1 - SIMBA 0.
Uimara wa kipa Mzungu, Obren Curkovic wa
Yanga, pamoja na kuwa na vurugu, imani za kishirikina na matukio
yakiwamo ya mashabiki kurusha uwanjani chupa za maji, na kadhalika... ni
baadhi ya matukio ambayo yalitawala mechi ya Ligi Kuu ya Vodacom
iliyomaliza karibu miaka minane ya ubabe wa Simba dhidi ya Yanga.

Katika mchezo huo ambao ulikuwa gumzo na
ubishi mkubwa miongoni mwa mashabiki,Yanga imefaulu kushinda kwa bao 1-0
katika Uwanja Mkuu wa Taifa,Dar es Salaam.

Mchezo huo uliokuwa wenye ushindani, ufundi
mkubwa kulinganisha na mechi nyingine zilizohusishwa katika ligi hiyo,
mwishowe Yanga walipata bao dakika ya 15 kupitia kwa Ben Mwalala baada
ya kupokea pasi ya Boniface Ambani ambaye aliwatoroka mabeki wa Simba na
kutingisha wavu.
|