![]() |
Your community website |
![]() |
||||||
|
|
|
|||||||
|
|
||||||||
|
|
||||||||
|
|
||||||||
|
NEWS |
||||||||
|
|
||||||||
Suleiman Salim (Morris) arudishwa Tanzania05/09/2008
MTANZANIA aliyekamatwa na makachero (FBI) wa Marekani kwa kuhusishwa na ugaidi, Suleiman Abdallah Salim (Morris) pichani, amerudishwa Zanzibar juzi na Shirika la Msalaba Mwekundu kutoka Afghanistan baada ya kubainika kwamba si gaidi. Akizungumza na Mwananchi nyumbani kwao maeneo ya Mombasa, Mkoa wa Mjini Magharibi Zanzibar, huku akionekana mchovu, alisema alikamatwa na makachero wa FBI nchini Somalia mwaka 2003 akiwa katika shughuli zake za kibiashara na kuingizwa katika gari bila ya kufahamu anapopelekwa. Akielezea mkasa uliomkuta akiwa eneo la Abusasu, mjini Mogadishu alisema baada ya kukamatwa na kuingizwa katika gari alisafirishwa hadi Nairobi, Kenya na kutakiwa apeleke mtu wa kudhamani, lakini aliwaambia kuwa yeye ni Mtanzania na hana kwamba ndugu yeyote jijini humo. “Waliniambia mimi ni Msomali nilikataa nikiwaambia kuwa ni Mtanzania. Kisha wakasema ni Myemen nikasema ni Mtanzania walipoona nasema Kiswahili wakananimbia mlete ndugu yako akuwekee dhamana, nikawaambia sina jamaa Nairobi mimi kwetu ni Tanzania,” alisimulia Salim. Alisema baadae alirejeshwa tena Somalia na kuwekwa kwenye kambi ya jeshi akiwa akiulizwa maswali mara kwa mara. Suleiman sasa amesharudishwa Tanzania. Habari ya Salma Said, Zanzibar.
|
||||||||
|
Custom Search
|
||||||||
|
|
|
|||||||
|
©
www.zenjydar.co.uk - Since 2007 |
|
||||||||