Mount Kilimanjaro

 

 

 

Your community website

Beit El Ajaib
     

HomeNewsServicesEventsAbout UsContact Us

ProfileToolsGamesCommunity

NEWS

 
 

Usipokumbuka Utaumbuka

10/09/2008

Mwenzangu! kama tumezoea kutupa uchafu na vikaratasi barabarani, tufikirie tena! Baraza la bara la Newham wameanzisha programu maalum ya kudumu kwa njia ya CCTV ambayo itawaangalia wale waliozoea kutupa-tupa vikaratasi barabarani.

Ukionekana kwenye CCTV kama umetupa uchafu, sura yako itatolewa na kuchapishwa kwenye gazeti maarufu la bara la Newham (Newham Mag) na kila mtu atakuona kwenye gazeti hilo likiwa likiomba msaada kama unamjua aliye pichani, ripoti kwenye mamlaka ili wamshughulikie na kumtoza faini ya £80.00. Gazeti la Newham Mag linawafikia karibu watu laki moja wanaoishi bara la Newham na kama kawaida yake hutolewa bila ya malipo kwa wakazi wa Newham.

Na endapo aliye kuwa pichani hajapatikana kwa muda maalum, mamlaka itafikiria kupeleka picha yake katika vyombo vingine vya habari vilivyopo hapa Newham. Newham ina CCTV zaidi ya 300.

Diwani wa Anti-social behaviour na Crime, barani Newham, June Leitch amesema, kuweka picha za wahalifu kwenye Newham Mag itapunguza idadi ya namba za uhalifu huo.

Kama unakabiliwa na Anti-social behaviour (utovu wa nidhamu) na vijana katika eneo lako, na hujui nini la kufanya, piga namba 0800 731 3300 kuripoti uhaini na utovu wa nidhamu.

 

   
 

Custom Search

Go up

 

Quick Links

Watch Television
Events Calendar
News Archive 2008
News Archive 2007

External Links

Alnoor CET
TZ Embassy UK
TZ's Community UK

© www.zenjydar.co.uk - Since 2007 | Web master | Site map | www.zenjydar.co.uk - Since 2007 ©